Ijumaa, 1 Julai 2016

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA YAKOPESHA MIL 80 VIJANA



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa imekopesha zaidi ya shilingi milioni 80 kwa vikundi 34 vya vijana kwa lengo la kukuza mtaji na kujiletea maeneleo kupitia shughuli za ujasiliamali.

Akisoma risala ya utii ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika mbio za Mwenge wa uhuru, Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Olgato Mwinuka alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015/2016 Halmashauri hiyo ilikusanya mapato ya ndani shilingi 1,201,059,165 na kutenga asilimia tano sawa na shilingi 85,724,000 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya vijana. 

Alisema “jumla ya fedha zilizotolewa ni shilingi 87,000,000 kati ya fedha hizi kiasi cha shilingi 30,000,000 zilitokana na asilimia tano ya mapato ya ndani, shilingi 37,000,000 zilitokana na mfuko wa vijana wa Halmashauri na shilingi 20,000,000 zilitokana na mkopo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo”. 

Alisema kuwa fedha hizo zilikopeshwa kwa vikundi 34 vya vijana vyenye jumla ya wanachama 361 (me 220 na ke 130) na kufanya kazi za uendeshaji miradi ya vijana katika kilimo cha mahindi, mpunga, alizeti, ufuta na mtama. Maeneo mengine aliyataja kuwa ni uselemala, ushonaji na ufugaji wa samaki, kuku, mbuzi na kondoo.    

Mwinuka alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa imeanzisha jumla ya vikundi 197 vya uzalishaji mali vya vijana waliosajiliwa vyenye jumla ya wanachama 1,811 (me 1,077 na ke 734).

Alisema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamewezesha vijana 651 (me 462 na ke 189) kupata mafunzo katika fani mbalimbali za ujasiliamali, stadi za maisha, kujitambua na kujikinga na maambukizi ya Ukimwi.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...