Alhamisi, 1 Machi 2018

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze kujiajiri kupitia viwanda.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya uzinduzi wa kongamano la kuhamasisha vijana kushiriki ujenzi wa Tanzania ya viwanda lililofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
Masenza alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa vijana na imetengeneza mazingira mazuri ya uwezeshaji mikopo yenye riba nafuu kwa vijana. Alisema kuwa uwezeshaji huo hufanyika kupitia mifuko mbalimbali ukiwemo, mfuko wa maendeleo ya vijana ambao upo halmashauri na mfuko wa wajasiriamali ambao upo SIDO. 

“Hivyo, nitoe rai kuwa mifuko hii itakuwa ni kichocheo na chanzo mojawapo ya mitaji kwa vijana ya kuanzishia viwanda Vidogo” alisema Masenza.

Akiongelea uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo, mkuu wa mkoa alisema kuwa mkoa una hali nzuri ya hewa inayoruhusu ustawi wa mazao ya aina mbalimbali ya chakula na biashara. Alisema kuwa mkoa una fursa za uwekezaji katika viwanda vya usindikaji wa matunda, mbogamboga, mazao ya nafaka na mafuta. 

Vingine ni viwanda vya kusindika maziwa, nyama na vyakula vya mifugo. Uwekezaji mwingine aliutaja kuwa katika viwanda vya kutengeneza zana za kilimo kama mashine za kuvunia mazao ya mpunga, mahindi na kupukuchua mahindi.

Kongamano la kuhamasisha vijana kujiingiza katika shughuli za uzalishaji katika sekta viwanda na biashara na uzinduzi wa kampeni yenye kaulimbiu ya ‘kijana hamasika, shiriki kikamilifu kuiunda Tanzania ya viwanda’.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...