Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Halmashauri
za mkoa wa Iringa zimetakiwa kuingiza wateja wote wa ardhi katika mfumo wa
ukusanyaji mapato ya ardhi wa kieletroniki ili serikali iweze kupata mapato
yake na kutoa huduza za kijamii.
Agizo
hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dr.
Angelina Mabula mjini Mafinga alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya
kikazi mkoani Iringa ya kukagua mifumo wa ukusanyaji mapayo ya ardhi mkoani
Iringa.
Dr.
Mabula alisema “Halmashauri zote
zimefungiwa mfumo wa ukusanyaji mapato, ila takwimu zao hazijakaa sawa.
Halmashauri hazijaweka utaratibu mzuri wa kuweka kumbukumbu. Hivyo, naagiza
kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2017, Halmashauri zote lazima wateja wake wote
wawe wameingizwa katika mfuko wa ukusanyaji mapato ya ardhi”.
Alisema kuwa
utaratibu wa kutoingiza wateja wote katika mfumo, unaikosesha serikali mapato
kwa sababu Halmashauri zinashindwa kuwatambua wateja wote wanaodaiwa. “Kutokana
na kushindwa kuwafahamu wateja wote, hata malengo yanayokadiliwa katika bajeti
yanakuwa chini sana ikilinganishwa na uhalisia” alisema Dr. Mabula.
Aliongeza
kuwa, Afisa Ardhi yeyote mteule, atakayeshindwa kufikia malengo ya kuingiza
wateja wote katika mfuko wa ukusanayaji mapato atatenguliwa nafasi yake na
nafasi hiyo kupewa mtu mwingine.
Naibu
Waziri alizishauri Halmashauri kuweka utaratibu wa kutoa notisi za kuwakumbusha
wateja wadaiwa wa kodi ya ardhi mara kwa mara ili kuwakumbusha kulipa tofauti
na utaratibu uliopo sasa.
Alisema
kuwa changamoto ya mfuko kushindwa kuwapata wateja wote wadaiwa kwa mara moja
imechukuliwa na wizara yake na itaenda kufaanyiwa kazi. Vilevile, alizitaka Halmashauri
kukusanya madeni yote ya ardhi kwa wateja ili fedha hizo ziweze kutumika katika
utaratibu wa serikali.
Akiongelea
ngogoro wa mpaka kati ya wilaya za Iringa na Kilolo, katika vijiji vya Ilole na
Ilambilole, Dr. Mabula alisemaa kuwa vijiji vyote vina GN jambo ambalo si la
kawaida. Aliagiza kuwa GN hizo zipitiwe upya ili kupatiwa suluhisho. Aliwataka
wakuu wa wilaya kuendelea kutatua migogoro iliyopo katika maeneo yao kwa
kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kusikiliza na kutatua kero zao.
Akiongelea
sababu za migogoro ya ardhi, Naibu Waziri alisema kuwa migogoro mingi ya ardhi
inachangiwa na kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kati ya wakuma na
wafugaji.
“Nazitaka Halmashauri kutambua idadi
ya wafugaji na mifugo waliyonayo ili kupanga matumizi bora ya ardhi”
aliagiza Naibu Waziri. Pia aliwataka wakuu wa wilaya kushiriki katika mikutano
ya ugawaji ardhi ili kusimamia taratibu zilizopo kufuatwa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni