Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkoa wa Iringa umepangiwa shilingi
15,614.372 milioni kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha
2016/2017.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji
wa matengenezo ya barabara na miradi ya maendeleo hadi kufikia tarehe 31 Disemba,
2016 katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika
ukumbi wa chuo Kikuu cha Mkwawa, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa
wa Iringa, Mhandisi Daniel Kindole, alisema “jumla ya shilingi 15,614.372
milioni zimepangwa kutumika katika miradi mbalimbali ya matengenezo na
ukarabati wa barabara mkoani Iringa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mhandisi Kindole alisema kuwa kati ya
fedha hizo, shilingi 13,896.372 zinatoka mfuko wa barabara na shilingi
1,718.000 zinatoka mfuko wa maendeleo.
Akielezea mchanganuo wa mpango wa
matengenezo kwa fedha za mfuko wa barabaara, Meneja wa TANROADS Mkoa alisema
kuwa barabara kuu zimetengewa shilingi 4,555.751 milioni kwa ajili ya matengenezo
maalumu ya madaraja matano (shilingi 188.800 milioni), matengenezo ya kinga ya
madaraja 140 (shilingi 140.000 milioni), matengenezo maalum kwa barabara za
changarawe/ udongo km 16.6 (shulingi 502.587 milioni), matengenezo maalum
barabara za lami km 3.8 (shilingi 1,683.853 milioni). Matengenezo mengine
aliyataja kuw ni matengenezo ya kawaida baraabara za changarawe/ udongo km 66.8
(shilingi 422.192 milioni) na matengenezo ya kawaida barabara ya lami km 317.5
(shilingi 1,618.319 milioni).
Akiongelea barabara za mikoa,
Mhandisi Kindole alisema kuwa matengenezo ya kawaida baraabara za lami, km 26.7
(shilingi 171.240 milioni), matengenezo ya kawaida barabara za chanagarawe/
udongo km 709.7 (shilingi 3,161.640 milioni), matengenezo maalum barabara za
lami km 3.5 (shilingi 1,540.980). Matengenezo mengine ni matengenezo maalum
barabara za changarawe/udongo km 158.3 (shilingi 3,843.528), matengenezo ya
kuboresha barabara za changarawe km 18.3 (shilingi 354.833 milioni),
matengenezo ya kinga ya madaraja 65 (shilingi 115.000 milioni) na matengenezo
maalum ya madaraja 7 (shilingi 153.400 milioni).
Kuhusu mpango wa ukarabati wa
barabara –miradi ya maendeleo, Meneja huyo alisema kuwa mpango huo utahusisha
ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara mbili km 0.7 kwa shilingi 362.000
milioni. Mpango mwingine ni ujenzi wa daraja (Lukosi II) shilingi 100.000
milioni, ukarabati wa kiwango cha lami km 0.3 kwa shilingi 250.000 milioni na
ukarabati wa kiwango cha changarawe kwa barabara nane kwa jumla ya km 52
shilingi 1006.000 milioni.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni