Jumapili, 23 Julai 2017

MKUU WA MAJESHI ATAKA USHIRIKIANO WA WANANCHI



Na. Mwandishi Maalum, Iringa
Jeshi la wananchi wa Tanzania limetaka ushirikino na wananchi katika kufichua wahalifu nchini.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Jenerali, Venance Mabeyo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ofisini kwake.

Jenerali Mabeyo aliupongeza mkoa wa Iringa kwa juhudi za kudumisha ulinzi na usalama. Aidha, alitoa wito kwa ushirikiano wa jamii nzima katika kulinda usalama wa nchini. “Ushirikiano wa vyombo vya usalama na ushirikiano wa wananchi ni muhimu sana kwa ulinzi wa nchi yetu” alisema Jenerali Mabeyo. 

Aidha, alisema kuwa adui asiyeonekana waziwazi wananchi wanawajibu wa kumfichua ili ashughulikiwe kwa sababu mara nyingi anakuwa miongoni mwa jamii kwa sababu wananchi wanawafahamu vizuri na wanaishi nao.

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa kamati yake ya ulinzi imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha mkoa unakuwa salama. “Maeneo ya kimkakati tunayangalia kwa makini. Vituo vya kibiashara pia tunavipa kipaombele katika ulinzi ili mkoa wetu uendelee kuwa salama” alisema Masenza.

=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...