Na
Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Redio
za ndani ya Mikoa zimetakiwa kijikita katika kutoa huduma ya habari za vijijini
ili wananchi hao wanufaike na huduma hizo.
Kauli
hiyo ilitolewa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambye ni Katibu Tawala Mkoa
wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akikagua banda la kituo cha redio cha Big
Star katika uwanja wa maonesho ya Nanenane wa John Mwakangale mjini Mbeya.
Wamoja
alisema kuwa redio za ndani zinawajabu wa kutoa huduma za habari zaidi
vijijini. Aliongeza kuwa vituo vingi vya redio vipo katika makao makuu ya miji
na masafa yake kuishia katika miji.
“Local
redio toeni huduza za habari za wananchi walio vijijini kwa sababu wanakosa
fursa za kupata habari. Wananchi walio katika miji wana nafuu kwa sababu redio
nyingi zinapatikana mjini na vyombo vingine vya habari vinapatikana huko kama
televisheni” alisisitiza Ayubu.
Aidha,
alivitaka vituo vya redio kuwaalika viongozi wa umma katika redio kusikiliza
kero za wananchi na kujibu hoja na maswali ya wananchi katika kuboresha utawala
bora. Aliongeza kuwa vituo vya redio vitapotenga muda kwa ajili ya viongozi
kusikiliza kero za wananchi kutasidia katika utatuzi wa kero na kuwawezesha
wananchi kuchapa kazi katika mazingira mazuri na rafiki.
“Endeleeni kuhabarisha wananchi kwa sababu wananchi wanawategemea na
kuwahitaji zaidi” alisisitiza Ayubu.
Kituo cha redio cha Big
Star kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2015 mjini Mbeya katika masafa ya
106.3 MHz kwa sasa redio hiyo inasikika katika mikoa ya Mbeya na Songwe, na
baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa na Ruvuma.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni