Jumatano, 4 Oktoba 2017

HALMASHAURI ZATAKIWA KUSHIRIKI MAONESHO YA UTALII KARIBU KUSINI



Na Dennis Gondwe, IRINGA
Halmashauri za mikoa ya nyanda za juu kusini zatakiwa kushiriki kikamilifu maonesho ya utalii karibu kusini ili kutangaza fursa za utalii na viwanda vidogo vilivyopo maeneo yao.

Kauli hiyi ilitolewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, kikanda na kimataifa Dr. Augustino Mahiga alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya wajasiriamali wa viwanda vidogo nyanda za juu kusini yaliyofanyika mjini Iringa.
 
Balozi Dr Augustino Mahiga
Dr. Mahiga alisema “natoa wito kwa halmashauri zote na wadau katika mikoa ya nyanda za juu kusini kuanza kujiandaa kikamilifu kushiriki katika maonesho haya ili kutumia nafasi hii kujitangaza na kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na viwanda”.

Waziri huyo aliwataka SIDO kufanya kazi kwa kujituma ili wajasiriamali waliojitokeza wabadilike na kuwa wafanyabiashara wakubwa. Aliongeza kuwaa wjasiriamali watakapobadilika na kuwa wafanya biashara wakubwa waendelee kuwasaidia wajasiriamali wengine ili wakue.

Dr. Mahiga alielezea matumaini yake kuwa maonesho ya mwaka 2018 yatakuwa yenye ufanisi mkubwa kwa kushirikisha wadau wengi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nchi jirani. “Tuzingatie tu kuwa utalii hauna mipaka na ni vema sasa tuanze kujitangaza pia kwa nchi jirani za Zambia, Malawi, msumbiji, na hata Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na kutumia balozi zetu za nje” alisema Dr. Mahiga.

Maadhimisho ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya shughuli za wajasiriamali wa SIDO yamehusisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mwanza, Pwani, Dar es Salaam, Geita, Lindi, Morogoro, Kilimanjaro, Tabora na nchi ya Kenya. Maonesho hayo yamehusisha mashine mbalimbali, bidhaa za usindikaji, bidhaa zilizosindikwa, bidhaa za ngozi, kazi za mikono na dawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...