Jumanne, 11 Februari 2014

WAMOJA AYUBU ASHUKURU USHIRIKIANO WA WATUMISHI




Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bibi. Wamoja Ayubu ameshukuru na kupongeza ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na taasisi mbalimbali zilizopo mkoani hapa kipindi akiwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

Kauli hiyo ameitoka katika mapokezi ya haja yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku yake ya kwanza ya kutumikia nafasi yake ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa baada ya uteuzi na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.

Bibi. Ayubu ameshukuru ushirikiano huo na kusema kuwa ushirikiano huo ndio uliomfanya kutekeleza vizuri majukumu yake akiwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Aidha, ametoa wito kwa watumishi wote na taasisi mbalimbali kuendelea kumpatia ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.

Akiongelea matarajio yake kwa wananchi wa mkoa wa Iringa, amesema kuwa hana wasiwasi na wananchi wa mkoa wa Iringa kutokana na uchapa kazi wao na kujituma katika kutekeleza majukumu ya serikali. Aisha, amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwake ili pamoja kuuletea maendeleo mkoa wa Iringa. 

Bibi. Wamoja ametumia fursa hiyo kushukuru ushirikiano aliopatiwa katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kilichofanyika mkoani Iringa.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atatekeleza majukumu yake kwa juhudi na maarifa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Uchumi na Sekta za Uzalishaji, Adam Swai ameutaja uteuzi uliofanywa na Rais Dkt. Kikwete kuwa ni faraja kubwa kwa watumishi na wananchi wa mkoa wa Iringa. Amemtaja Bibi. Ayubu kuwa ni mchapa kazi mzuri anayetoa ushauri mzuri kwa watumishi walio chini yake. 

Aidha, amewataka watumishi na viongozi wote kumpatia ushirikiano unaostahili hasa katika kindi hiki ambapo mkoa wa Iringa unahitaji kuzalisha chakula kwa wingi.

Ikumbukwe kuwa Bibi. Wamoja Ayubu anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa akipokea kijiti kutoka kwa Katibu Tawala Mstaafu Bibi. Gertrude Mpaka aliyestaafu mwaka 2012.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...