Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
29/03/2014
Na.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Zaidi
ya 5% ya wanandoa wameambukizwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini wakati
asilimia 29 ya wanaume wanakadiriwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa.
Kauli
hiyo imetolawa na Simon Keraryo, kutoka TACAIDS alipokuwa aliwasilisha mada juu
ya mwenendo wa Ukimwi nchini katika "Media Orientation" iliyofanyika
katika hoteli ya Kalenga West Park mjini Iringa.
Keraryo
amesema kuwa pamoja na kushuka kwa maambukizi ya Ukimwi, bado kuna changamoto
kubwa katika udhibiti wa Ukimwi nchini katika maambukizi mapya. Amesema kuwa
inakadiriwa zaidi ya watu 100,000 wanaambukizwa Ukimwi kila mwaka.
Amesema kuwa
hali hio inasababishwa na tabia zenye kuchangia maambukizi. Akitolea mfano
mwaka 2008 asilimia 18 ya wanaume na asilimia tatu ya wanawake waliripotiwa
kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja nchini. Amesema
kuwa kiwango hicho kimeongezeka hadi kufikia 21% ya wanaume na asilimia nne kwa
wanawake 2012.
Kuhusu
uhusiano nje ya ndoa, Keraryo amesema kuwa 29% ya wanaume na 16% ya wanawake
wanakadiriwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa. Ameongeza kuwa inakadiriwa kuwa
asilimia 5.3 ya wanandoa wameambukizwa virusi vya Ukimwi.
Akiongelea
hali ya maambuki ya Ukimwi nchini, Keraryo amesema kuwa kiwango cha ushamiri wa
VVU kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/2004 hadi kufikia asilimia 5.3 mwaka
2011/2012. Amesema kuwa kiwango cha maambukizi kimeshuka kwa wanaume kutoka
asilimia 6.3 mwaka 2003/2004 hadi kufikia asilimia 3.9 mwaka 2011/2012.
Akiongelea
maambukizi kwa makundi maalumu, amesema kuwa maambukizi ni makubwa kwa wauza
ngono na wateja wao kufikia 31.4%. amesema kuwa wanaume wanaofanya ngono wao kwa
wao ni 41% na 34.8% watu wanaojidunga dawa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni