Zainab Maeda.
Iringa,
WAKAZI wapatao 2379 wa kijiji cha
Ikuka katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambao walikuwa
wanalazimika kutembea umbali mrefu kupata huduma ya maji safi na salama toka
Uhuru wa Taifa hili sasa wanatarajia kupata huduma hiyo baada ya
kukamilika kwa mradiu mkubwa wa maji kijijini hapo.
Akisoma taarifa ya mradi huo
mhandisi wa maji wilaya ya Kilolo katika siku ya maadhimisho ya kilele
cha wiki ya maji , Enock Basyegile alisema kuwa wakazi wa kijiji hicho
wanatarajia kupata huduma hiyo ya maji safi na salama endapo mradi huo
utakamilika kwa wakati.
Alisema kuwa mradi huo
umegharimu zaidi ya milioni 400 unatarajiwa kumalizika juni 30 mwaka huu
ambapo bado kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 11 ilii kukamilika kwa mradi
Alisema kuwa mradi huu unatekelezwa
chini chini ya miradi ya Matokeo Makubwa sasa (BRN).
“Mradi huu ulianza juni 26 mwaka 2013
na unatarajia kuwa mradi huu utakamilika juni 30 mwaka huu,ili kukamilika kwa
mradi huu zaidi ya shilingi 11 milioni zinahitajika ili wananchi waweze kupata
huduma hii kwa wakati unaotakiwa”Alisema Basyegile.
Naye mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa
Iringa wakati akizindua mradi huo Gerald Guninita aliwataka wakazi wa kijiji
hicho kuutunza mradi huo ili uwe endelevu.
Guninita ambaye pia ni mkuu wa wilaya
ya Kilolo alisema kuwa jukumu la kulinda mradi huo ni la wananchi wenyewe ambao
ndio walengwa wa matumizi ya maji safi na salama.
“Wakazi wa kijiji cha Ikuka mnatakiwa
kuutunza mradi huu ikiwa ni pamoja na kuyatunza mazingira na vyanzo vya maji
ili muweze kunufaika na kuufanya mradi kuwa endelevu”alisema Guninita na
kuongeza kuwa.
“Sheria na hatua zitachukuliwa kwa
atakaebainika kufanya uharibifu wa mradi huo kama vile wizi wa mambomba na
vinginevyo vilivyopo katika mradi”
Wananchi wanaopata huduma ya maji
safi na salama mijini katika mkoa wa Iringa ni 189,644 kati ya wananchi 247,156
ambao ni sawa na asilimia 76.7 ya wananchi waishio mijini.
Hali ya huduma ya maji mijini
inategemewa kuongezeka mara baada ya kutekelezwa kwa miradikatika miji ya
Ilula,Kilolo,na Mafinga,na miradi hii inategemewa kutekelezwa kupitia program
ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP) ambapo jumla ya wananchi 57,512 watapata
huduma bora ya majisafi na salama.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni