VIONGOZI wa dini, watumishi wa
serikali na waandishi wa habari mkoani Iringa wametakiwa kusaidia katika kuhamasisha,
zoezi la chanjo ya surua dozi, ya pili inayotarajiwa kuanza mei mosi,
ikiwahusisha watoto wenye umri wa miezi 18.
Rai hiyo imetolewa leo mkoani
Iringa, wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa wa katibu tawala,
mkoani Iringa.
Akitoa mafunzo hayo, Mratibu wa
afya ya uzazi na mtoto mkoani Iringa, Mariam Mohamed amesema mbali na mafunzo
kwa makundi hayo tayari, wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za
afya za vijiji, mitaa na kata na wilaya ili kuongeza uelewa juu ya chanjo hiyo.
Aliitaka jamii kuondoa dhana
finyu kuhusiana na chanjo, kwa madai kuwa lengo la zoezi hilo ni kuendelea kupambana na virusi vinavyosababisha
ugonjwa wa surua ambao hivi sasa ni tishio kwa watoto.
“Surua ni ugonjwa hatari
unaosababishwa na virusi vya surua hivyo chanjoa ya surua ni muhimu kwa watoto
kwani inaubora uliothibitishwa na wizara
ya afya na ustawi wa jamii na shirika la afya ulimwenguni..ni salama,”
alisema..
Aliwataka wazazi na walezi
kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze
kupatiwa chanjo hiyo.
@MUITIKIO BLOG
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni