Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Vijana
nchini wametakiwa kuwekeza katika miradi ya utunzaji wa mazingira ili taifa
liweze kuwa mahali salama kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.
Kauli
hiyo imetolewa kiongozi wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2014 Rachel Kassanda
baada ya kuzindua mradi wa hifadhi ya mazingira na kukagua mradi wa ufugaji wa
nyuki wa vijana na kutundika mizinga katika kijiji cha kinyanambo ‘C’ wilayani
Mufindi.
Kassanda
amesema kuwa umefika wakati kwa vijana nchini kubuni miradi ya utunzaji wa mazingira.
Amesema kuwa miradi ya utunzaji wa mazingira na ufugaji nyuki ni miradi yenye
tija kwa muda mrefu kwa vijana na kwa taifa kwa ujumla. Amewapongeza vijana hao
kwa kubuni miradi hiyo inayowawezesha kujiongezea kipato na kutunza mazingira.
Katika
taarifa fupi ya mradi wa hifadhi ya mazingira na ufugaji nyuki wa vijana
imetaarifiwa kuwa lengo la mradi huo wa upandaji miti na ufugaji nyuki ni
kuhifadhi mazingira na kuwekeza katika sekta ya misitu na nyuki ili kuweza
kujikwamua kiuchumi.
Akiongelea
gharama katibu wa kikundi Violeth Matala amesema kuwa miradi yote ya upandaji
wa miti na ufugaji wa nyuki imegharimu shilingi 48,333,330. Ameutaja mchanganuo
wake kuwa ni mradi wa upandaji miti shilingi 45,683,330 kwa lengo la kukunua
ardhi, upandaji na gharama za utunzaji. Amesema kuwa mradi wa ufugaji nyuki
shilingi 2,650,000 kwa ajili ya ununuzi wa mizinga usharifishaji na utunzaji wa
shamba. Amesema kuwa halmashauri ya wilaya imechangia shilingi 500,000/= kwa
ununuzi wa mizinga ya kisasa.
Shamba
hilo lina hekari 20 lililopandwa mikaratusi likiwa na mizinga 55 hadi sasa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni