Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
Rachel Kassanda amewapongeza wakinamama wa kikundi cha Tuinuane kwa kazi za
kujiongezea kipato na kukabiliana na umasikini.
Kassanda ameyasema hayo alipokuwa
akizindua kikundi hicho na kukabidhi hundi ya shilingi 1,000,000 ukiwa ni
mchango kutoka halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa lengo la kukiongezea mtaji
kikundi hicho ili kiweze kujitegemea.
Amepongeza juhudi za kujiongezea
kipato kupitia utaratibu wa hisa ambapo wanachana waliweza kukusanya kiasi cha
shilingi 240,000 na kujiunga na Mazombe SACCOS hatimaye kupata mkopo wa
shilingi 4,400,000.
Akiwasilisha taarifa ya kikundi cha
wanawake Tuinuane, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Masukanzi Jumanne Tembo amesema
kuwa kikundi hicho kilianza mwaka 2012 kikiwa na wanachama 23. Amesema kuwa
kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwaongezea kipato wanakikundi.
Tembo amesema kuwa kikundi hicho
kimefaidika na mradi wa Corridor Economic Empowerment Project (CEEP) kuwapatia
elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni