Jumatatu, 30 Juni 2014

VIONGOZI WAANZA KUWASILI IRINGA KUHUDHURIA JUBILEI YA ASKOFU NGALALEKUMTWA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkoa wa Iringa umeanza kupokea viongozi mbalimbali wanaoshiriki katika Jubilei ya miaka 25 ya Mhashamu Baba Askofu Tarcisius JM. Ngalalekumtwa (1989-2014). 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (kushoto) akimkaribisha mkoani Iringa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa alipowasili uwanja wa Ndege wa Iringa

Miongoni wa wageni mashuhuru waliowasili mkoani hapa ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa aliyewasili majira ya saa 10 jioni na Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb.), Spika wa Bunge la Tanzania.

Viongozi wengine waliowasili mkoani hapa ni Mawaziri, viongozi wa kisiasa na Maaskofu na Makasisi wa kikatoliki.

Jubilei hiyo ya kutimiza miaka 25 ya uaskofu itatanguliwa na misa takatifu ya shukrani itakayofanyika katika kanisa katoliki Kihesa.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...