Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma amefutarisha wananchi kwa lengo la
kujenga umoja na kuaminiana ili kudumisha amani na utulivu.
Futari kwa akina mama |
Kauli
hiyo ameitoa alipokuwa akiongea na waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa
ujumla waliohudhuria futari hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo iliyopo mjini
Iringa. Amesema “lengo la kuandaa futari hii ni kutuweka pamoja kwa lengo la
kujenga na kudumisha umoja wetu”.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa amewataka viongozi wote wa dini kutumia muda wao kuuombea
Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla ili amani ya kudumu iendelee kushamiri
nchini.
Akiongelea
wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Dkt. Ishengoma amesema kuwa
hata wale wasiotaka kurudi bungeni waombewe ili waweze kurudi bungeni. Amesema
kuwa tofauti na kutokuelewana kunatatuliwa kupitia vikao na meza ya
majadiliano.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni