Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Wilaya
zimetakiwa kubuni mipango ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana ili waweze
kujiajiri na kujiletea maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa
akikabidhiwa mashine 16 za kufyatulia matofali kutoka shirika la nyumba la
Taifa (NHC) katika uwanja wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. christine Ishengoma akipokea mashine za kutengeneza tofali toka kwa Meneja wa NHC Iringa |
Dkt.
Ishengoma amesema “natumia fursa hii kutoa wito kwa wilaya na halmashauri zote
kubuni mipango ambayo itawezesha kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa haraka
kama ilivyo kwa mradi huu wa kufyatua tofali”. Amewataka msaada huo uliotolewa
uwe ni changamoto kwao kuendelea kuunda vikundi vya uzalishaji mali vya vijana
nan kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo ya vijana.
Aidha, amezitaka halmashauri kuongeza vikundi vingi na kuwanunulia vijana
mashine za kutengenezea matofali na kuvikopesha vikundi hivyo kwa lengo la
kuvifanya endelevu.
Akiongelea
vijana waliochaguliwa kupata msaada wa mafunzo na mashine hizo 16, Mkuu wa Mkoa
wa Iringa amewataka vijana hao kuzitunza vizuri mashine hizo kama mafunzo
waliyopewa. Amesema kuwa serikali inategemea kuona hali za kimaisha za vijana
hao zinabadilika na kuwa bora sambamba na vikundi kuimarika. Amewataka kutumia
fursa hiyo ya kupewa mashine hizo kama chachu ya kuonesha uwezo na ubunifu
zaidi. Amesema kuwa kufanya kwao vizuri kutawafanya vijana wengine kwenda
kujifunza kwao kwa lengo la kuwa na uelewa mpana.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni