Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Baraza
la Maaskofu Katoliki limewataka wajumbe wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)
kurejea bunguni bila masharti ili kuhakikisha mchakato wa upatikanaji wa katiba
mpya unafanikiwa.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania Askofu
Severine Niwemugizi katika hotuba yake baada ya misa takatifu ya sherehe ya
jubilei ya miaka 25 ya uaskofu wa Mhashamu Tarcisius JM. Ngalalekumtwa
iliyofanyika katika kanisa katoliki la Kihesa.
Severine Niwemugizi, Makamu Mwenyekiti wa TEC |
Askofu
Niwemugizi amewataka wajumbe wote wanaounda umoja wa katiba ya wananchi kurudi
bungeni mwezi ujao pasipo masharti yoyote. Amesema kuwa wajumbe hao warudi
bungeni na kujadili rasimu ya pili ya katiba mpya kwa mujibu wa sheria. Amesema
kuwa jukumu hilo ndilo walilotumwa kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Katika
hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema
kuwa serikali itaendelea kuthamini na kuunga mkono mchango wa taasisi za kidini
katika kuleta maendeleo nchini. Amesema kuwa taasisi za kidini zimekuwa
zikichangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji na uboreshaji wa huduma katika
nyanja za elimu, afya malezi na mambo mengine kama hayo.
Akiwatambulisha
wageni waliohudhuria misa ya jubilei, mkuu wa mkoa wa Iringa, Dkt. Christine
Ishengoma amesema kuwa mkoa wa Iringa unautulivu na usalama wa kutosha. Amesema
kuwa mkoa unajivunia ukarimu wa wananchi wake jambo litakalowafanya wageni
kufurahia uwepo wao mkoani Iringa.
Amempongeza
baba Askofu Ngalalekumtwa kwa kutimiza miaka 25 ya uaskofu na kumtakia maisha
marefu zaidi ili aendelee kuwahudumia watanzania kiroho.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni