Sekta
ya kilimo inayochangia zaidi ya asilimia 24 ya pato la taifa imejizatiti
kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa kuongeza uzalishaji wa mahindi na mpunga
ili kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuuza nje ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na waziri wa kilimo, chakula na ushirika, Mhandisi. Christiper
Chiza alipokuwa akihutubia wananchi na wadau wa sekta hiyo katika siku maalum
ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) katika kilimo iliyotolewa kituo cha
mafunzo ya wakulima Mkindo, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi. Christopher Chiza |
Mhandisi.
Chiza amesema “sekta ya kilimo inachangia kwa asilimia 24.5 ya pato la Taifa;
inachangia zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya chakula nchini; inatoa ajira
kwa wastani wa asilimia 74 ya watanzania; inachangia kwa asilimia 33 ya fedha
za kigeni; na ni chanzo kikubwa cha malighafi kwa viwanda vyetu vya ndani”.
Amesema
kuwa hadi kufikia mwaka 2016, mpango wa matokeo makubwa sasa utafanikisha
ongezeko kwa uzalishaji wa mahindi kwa tani 100,000 kutoka tani milioni 3.4 kwa
mwaka. Amesema kuwa sekta inalenga ongezeko la kuzalisha mpunga kwa tani
290,000 kutoka tani milioni 1.3 zinazozalishwa sasa.
Maeneo
mengine ameyataja kuwa ni pamoja na kuendeleza eneo jipya la kilimo cha
kibiashara hekta 350,000 na kuboresha eneo la wakulima wadogo hekta 330,000.
Maeneo mengine ni kuongeza uzalishaji wa sukari kwa tani 150,000 na kuongeza
idadi ya wakulima watakaoshiriki kuwa zaidi ya 400,000.
Waziri
wa kilimo, chakula na ushirika amesema kuwa utekelezaji wa mpango wa matokeo
makubwa sasa kwa mwaka 2014/ 2015 utakuwa katika maeneo ya kuendeleza mashamba
8 ya kilimo cha kibiashara cha miwa na mpunga. Eneo lingine amelitaja kuwa ni
kuboresha skimu 39 za umwagiliaji mpunga kwa kujenga miundo mbinu ya
umwagiliaji na maghala kwa ajili ya uhifadhi wa mpunga ili kurahisisha
upatikanaji wa masoko na kuboresha maghala 145 kwa ajili ya uhifadhi wa mahindi
ili kurahisisha upatikanaji wa masoko.
Mwakilishi
wa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo, Dkt.
Christine Ishengoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Iringa amesema kuwa umefika
wakati kwa vijana kujikita katika shughuli za kilimo nchini. Amesema kuwa
kamati yake itaendelea kushauri kuboreshwa kwa mazingira mazuri katika sekta ya
kilimo ili kuwavutia vijana wengi kujikita katika sekta ya kilimo. Amesema kuwa
mazingira mazuri yatachangia ajira kwa vijana na kukuza pato la kaya na taifa
kwa ujumla.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Maji na Mifugo Dkt. Chhristine Ishengoma (Mb.) |
Rozina
Mkude ambaye ni mkulima wa mpunga katika kijiji cha mkindo wilayani Mvomero
amepongeza jihudi za serikali kukuza sekta ya kilimo nchini. Amesema mpango wa
sasa wa kukifanya kilimo kiwe cha kibiashara utasaidia kukuza kipato cha
familia na kuondoa umasikini kupitia sekta ya kilimo. Amesema kuwa ni mara ya
kwanza kwa sehere hizo kufanyika kijijini na kuwahusisha wananchi wengi ambao
ndio wakulima halisi tofauti na wakulima wa vitabuni.
Sekta
ya kilimo inakuwa kwa wastani wa asilimia nne kwa muongo mmoja sasa ikiongozwa
na kaulimbiu isemayo matokeo makubwa sasa, kilimo ni biashara.
Mashine ya Mpunga |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni