Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkoa wa Iringa umepata kibali cha
kumiliki na kuendeleza jengo la kale lililojengwa na utawala wa kijerumani
maarufu kama Iringa Boma.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala
Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu
ukaratabi wa wa jengo la zamani la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iringa ambalo
litakuwa makumbusho ya Mkoa baada ya kukamilika. Taarifa hiyo ilitolewa katika
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Wamoja amesema “nimefurahi sana kwa
kupata fursa hii adhimu kutangaza rasmi kuwa mkoa wetu umepata kibali
kilichongojewa kwa muda mrefu cha kumiliki na kuendeleza jengo la kale
lililojengwa na utawala wa kijerumani lenye umri wa miaka 114, maarufu kama
Iringa Boma.” Amesema kuwa kibali hicho kimetolewa na wizara ya maliasili na
utalii.
Amesema kuwa lengo ni kulibadilijengo
hilo na kulitumia kama jumba la makumbusho. Amesema kuwa watakusanya na kuweka
kumbukumbu, kufanya maonesho mbalimbali ya urithi na utamaduni wa Mkoa wa
Iringa kwa lengo la kukuza utalii na kuleta maendeleo endelevu. “urithi wetu na
utamaduni wetu ni uti wa mgongo wa utambulisho wetu kama wanadamu. Kuwepo kwa
lugha anuai, tamaduni, dini, muziki pamoja na ala mbalimbali za muziki, kazi za
sanaa na jinsi tunavyoishi inaashiria na kuthibitisha dhahiri urithi wa mila
zetu mbalimbali.” Alisisitiza Wamoja.
Iringa Boma |
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni