SALAMU ZA MKUU WA MKOA WA IRINGA,
MHESHIMIWA AMINA JUMA MASENZA ZA KUWATAKIA HERI WANANCHI WA MKOA WA IRINGA
KATIKA SHEREHE ZA NOELI NA MWAKA MPYA 2015 TAREHE 24/12/2014
Ndugu
Wananchi wa Mkoa wa Iringa
Ninayo
heshima kubwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha tuwe na afya njema tokea
tulipoanza mwaka 2014. Ni matumaini yangu kuwa Mungu atatuwezesha pia kuumaliza
salama mwaka 2014 na hatimae kuuanza mwaka 2015.
Aidha,
napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kwa ushiriki
wenu katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Ndugu
Wananchi,
Katika
kipindi chote cha mwaka 2014 wananchi wa Mkoa wa Iringa mmekuwa mkifanya kazi
kwa kujituma na kwa ushirikiano mkubwa. Ni matumaini yangu kwamba tabia hii ya
kufanya kazi kwa kujituma na mshikamano itaendelea Mwaka 2015. Kufanya kazi kwa kujituma na mshikamano
kutaleta tija na maendelo ya mwananchi mmoja mmoja na Mkoa wa Iringa kwa
ujumla.
Ndugu
wananchi;
Msimu
wa kilimo tayari umeanza. Nitoe wito kwenu kuzitumia vizuri mvua zinazo endelea
kunyesha. Muda huu ni muda muafaka wa kupanda mazao ili kujihakikishia uhakika
wa chakula.
Katika maeneo yenye uzoefu wa kupata mvua
chache hususani Mahenge, Isimani, pandeni mazao yanayovumilia ukame. Aidha, tukumbuke kupanda miti katika Msimu
huu wa mvua kwa kuwa Mkoa wetu unahali ya hewa nzuri inayostawisha miti.
Ndugu wananchi;
Tunapopanda mazao mbalimbali tumieni mbegu
bora, mbolea ya kupandia na kukuzia hasa kwa kilimo cha Mahindi na Mpunga ili
kupata mazao bora. Wahenga walinena kuwa “Mvua ya kwanza ni mvua ya kupandia”
Ndugu
Wananchi; Ulinzi na Usalama
Nawaomba
sana ndugu zangu wananchi wa Mkoa wa Iringa, kwa umoja wetu tuhakikishe
tunasimamia na kudumisha Ulinzi na Usalama ili Mkoa wetu uendelee kuwa na amani
na utulivu. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunatokomeza kabisa vitendo vyote
vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika Mkoa wetu wa Iringa na nchi yetu kwa
ujumla. Sote tujikite kwenye shughuli za maendeleo na kudumisha umoja. Hali ya usalama ya Mkoa ni shwari na Vyombo
vyote vya Dola vitaendelea kuwa makini katika kusimamia amani na utulivu katika
Mkoa wa Iringa ili wananchi waweze kushiriki katika shughuli zao za kujiletea
maendeleo.
Salamu za Noeli na Mwaka Mpya 2015
Ndugu
Wananchi;
Napenda kuwatakia sikukuu njema ya Noeli
na Mwaka Mpya 2015 wenye mafanikio tele. Ninawasihi kuhakikisha mnasherehekea
sikukuu hizi kwa amani, usalama na utulivu.
Serikali itahakikisha ulinzi na usalama
vinakuwepo kipindi chote cha sikukuu kwa sababu uzoefu unaonesha kuwa katika
majira ya sikukuu watu wasiopenda kuona amani na utulivu wa Mkoa hutumia majira
haya kufanya uhalifu. Ulinzi uanzie
ngazi ya kaya, kila mwanafamilia awe makini na kutoa taarifa anapokuwa na
wasiwasi na jambo linaloweza kuhatarisha amani na usalama wake na wa Mkoa kwa
ujumla.
Wazazi, kipindi hiki cha Sikukuu ni
kipindi muafaka cha kukaa na familia kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapokwenda.
Ni wakati muafaka wa kupanga malengo ya familia na namna ya kuyafikia.
Mwisho,
Mvua
zinaendelea kunyesha zimeanza kusababisha maafa, hivyo nawasihi wananchi wote
kuchukua tahadhari, hususani wanaoishi mabondeni naomba wahame maeneo hayo.
Ndugu
wananchi,
Baada
ya kusema haya asanteni kwa kunisikiliza na nawatakia Sikukuu njema ya Chrismas
na Mwaka Mpya (2015).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni