Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Matokeo ya ufaulu kwa mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi mwaka 2014 ni mazuri ikilinganishwa na mwaka 2013
pamoja na Mkoa wa Iringa kushika nafasi ya nne kitaifa.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu wa
Mkoa wa Iringa, Mwl. Joseph Mnyikambi alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya mwelekeo
wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2014 kwa Mkoa wa Iringa
katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza katika
Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
Mwl. Mnyikambi amesema, “Matokeo kwa
ujumla kimkoa ni mazuri. Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa Halmashauri zote.”
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kulia) na Afisa Elimu Mkoa wa Iringa, Mwl. Joseph Mnyikambi (kushoto |
Akiongelea hali ya matokeo kimkoa,
amesema kuwa jumla ya shule za msingi 458 zenye watahiniwa 21,363 walifanya
mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2014. Amesema kuwa hali ya ufaulu
imeongezeka katika halmashauri ikilinganishwa na mwaka 2013. Iringa (M) ufaulu
umeongezeka 0.59%, Iringa 5.97%, Kilolo 03%, na Mufindi 4.31%.
Afisa elimu huyo amesema kuwa mahudhurio
ya wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi
mwaka 2014 yameongezeka kwa 0.18%. Amesema kuwa mwaka 2013 mahudhurio siku za
mitihani yalikuwa 99.02% hadi kufikia 99.2% mwaka 2014.
Mwl. Mnyikambi ameelezea utaratibu wa
kutangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi mwaka 2014 yanatangazwa baada ya kutangazwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ngazi ya kitaifa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni