Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shule
ya sekondari Kihesa imetakiwa kujipanga vizuri kuhakikisha wanafunzi wanafaulu
zaidi katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2015.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akiongea na uongozi wa
shule ya sekondari Kihesa na wananchi waliohudhuria tukio hilo la ukazugi wa
ujenzi wa Maabara.
Waziri
Mkuu ameitaka shule ya sekondari Kihesa yenye mikondo minne ya kidato cha nne
iliwa na jumla ya wanafunzi 170 kuhakikisha angalau mikondo miwili wanapata
daraja la kwanza katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka huu 2015.
Kauli
hiyo imetokana na waziri Mkuu kutoridhishwa kiwango cha ufauli wa shule hiyo
kwa matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo. Kwa mwaka 2012 na
2013 hapakuwa na daraja la kwanza wakati daraja pili walikuwa wawili (2012) na
sita (2013) wakati daraja la tatu walikuwa saba (2012) na 24 (2013). Kwa mwaka
2014 daraja la kwanza alikuwa mmoja, la pili 12 na la tatu 20. Amesema kuwa
matokeo hayo hayaridhishi kwa shule iliyo katika manispaa ya Iringa. Amesema
kuwa shule hizo zina miundombinu imara na mazingira bora ya kusomea na
kujifunzia.
Katika
taarifa ya ujenzi wa Maabara katika shule ya sekondari ya Kihesa iliyosomwa kwa
Waziri Mkuu na Mkuu wa shule ya sekondari Kihesa, Bwana Hudson Luhwago amesema
kuwa ujenzi wa vyumba vya Maabara tatu, maboma yamekamilika na hatua
inayoendelea ni ukamilishaji wa miundombinu ya ndani. Akiongelea gharama
amesema kuwa hadi kukamilika kwake ujenzi huo unatarajia kugharimu shilingi
170,195,920. Amesema kuwa gharama hizo zinatokana na wastani wa shilingi
56,731,973 kwa Maabara moja. Amesema kuwa gharama hizo zimepungua kutokana na
kutumia nguvu za wananchi na wadau mbalimbali.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni