Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Kazi ya kuboresha maisha ya
watanzania ni jukumu la wadau wote wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Mhe. Amina Masenza katika hotuba yake iliyosomwa na Mrajisi Msaidizi
wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Iringa, Bw. John Kiteve katika sherehe za
uzinduzi wa Mnara mpya wa Tigi uliopo kijiji cha Magubike, Wilayani Iringa.
Mhe. Masenza amesema “kazi ya
kuboresha maisha ya watanzania si jukumu la serikali peke yake bali ni la wadau
wote wa maendeleo wakiwemo kampuni za simu nchini jama wanavyofanya wenzetu wa
Tigo”. Amesema kuwa kwa sababu hiyo
kupitia mpango wa universal communications services access fund (UCSAF)
serikali imekuwa ikishirikiana na kampuni za simu jupanua upatikanaji wa huduma
za mawasiliano nchini hadi vijijini. Amesema kuwa mnara uliozinduliwa katika
kijiji cha Magubike ni miongoni mwa minara inayojengwa kwa pamoja kati ya
serikali na kampuni za simu katika sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa mkoa waliwahakikishia wawekezaji
katika sekta ya mawasiliano kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao pamoja na
wadau wengine wa maendeleo kwa kuweka mazingira bora ya utendaji kazi kwa
madhumuni ya kuboresha sekta ya mawasiliano nchini. Amesema kuwa serikali
inatambua kuwa uwekezaji katika huduma za mawasiliano utaleta maendeleo ya
haraka katika sekta nyingine za uzalishaji kama kilimo, utalii, uchimbaji
madini na biashara kwa maendeleo ya taifa.
Kutokana na huduma za mawasiliano ya
simu kwa kiasi kikubwa kuwa maeneo ya mjini, Mhe. Masenza ameelezea faraja
aliyopata kwa juhudi za kampuni ya Tigo kuendelea kufikisha huduma za
mawasiliano ya simu vijijini. “Naipongeza sana kampuni ya Tigo kwa juhudi hizi
na kuiomba iendelee kutekeleza mpango huu mzuri kwa taifa letu” alisisitiza Mhe.
Masenza.
Amesema kuwa kwa mkakati huo wa
kufikisha huduma za mawasiliano ya simu vijijini, Tigo inaendelea kuwa mdau
muhimu katika kuchangia uboreshaji maisha ya wananchi wa Tanzania ikiwa ni
sehemu ya kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kukuza
Uchumi Tanzania na Mpango wa Maendeleo ya Milenia.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni