Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Maafisa rasilimali watu watakiwa
kuwaelimisha waajiriwa wapya juu ya sheria inayowapa uhuru wa kuchagua mfuko wa
hifadhi wanaoupenda.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Mhe. Amina Masenza katika hotuba yake ya ufunguzi wa semina
iliyosomwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Iringa, Bw. John
Kiteve kwa maafisa rasilimali watu waliopo mkoani Iringa iliyofanyika katika
ukumbi wa hoteli ya Gentle Hills Manispaa ya Iringa.
Mhe. Masenza amesema kuwa ipo sheria
inayotoa nafasi kwa waajiriwa wapya kufanya chagua la mfuko wa hifadhi ya jamii
wanaoupenda na kuchangia katika kipindi cha ajira zao. Amesema kuwa sheria hiyo
hairuhusu kwa mwajiriwa kuhama mfuko baada ya kuuchagua. “Hivyo ninyi kama
waajiri na walezi wao mnayo dhamana ya kuwashauri juu ya ukweli huu ili
wafahamu wanapoenda kufanya chaguo” alisisitiza Mhe. Masenza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliapongeza
GEPF kwa kuandaa semina hiyo na kuwataka kufanya semina hizo mara kwa mara ili
kuweza kwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea kwa kasi katika sekta ya
hifadhi ya Jamii nchini. Amewakumbusha kuwa elimu haina mwisho na kuwataka
kuwafahamisha wadau kila linapotokea jambo jipya ili wato wafahamu na kwenda
kapoja katika kulifanikisha.
Mkuu wa mkoa amepongeza juhudi za
GEPF kuwakopesha wananchama wake. Amesema “mfuko wa GEPF umekuwa ukiwakopesha wanachama
wake kwa kipindi kirefu sana, kupitia mikopo hii mwanachama anaweza kuchukua
mpaka 45% ya mafao yake jambo ambalo ni msaada mkubwa kwa wanachama”.
Mkuu wa mkoa ameutaka mfuko wa
hifadhi wa GEPF kutoa huduma bora kwa wateja. Amewataka kuutekeleza mkataba wa
huduma kwa mteja kwa vitendo ili ulete maana. Aidha, amewataka kuimarisha mfumo
wa utoaji taarifa kwa wanachama na matumizi ya Tehama.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni