Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mikoa ya Iringa na Njombe ina asilimia
81.9 ya watu wanaojua kusoma na kuandika.
Akitoa taarifa ya Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kwa mikoa ya Iringa na Njombe kwa waandishi wa habari ofisini kwake,
Meneja wa Takwimu (M) Iringa/ Njombe, Bw. Fabian Fundi amesema kuwa kwa mujibu
wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, mkoa wa Iringa una asilimia 81.9 ya
watu wanaojua kusoma na kuandika. Amewataja wanaume ni 88.4 na wanawake 76.1, watu wasiojua kusoma na
kuandika asilimia 18.1, wanaume 11.6 na wanawake 23.9. Aidha, mkoa wa Njombe una
asilimia 81.9 ya watu wanaojua kusoma na kuandika, wanaume wakiwa 88.1 na
wanawake 76.8, watu wasiojua kusoma na kuandika asilimia 18.1, wanaume 11.9 na
wanawake 23.2.
Akiongelea elimu ya msingi, Meneja wa
Takwimu (M) Iringa/ Njombe, amesema “kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya
mwaka 2012 imeainisha uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi. Mkoa wa
Iringa waliandikishwa wanafunzi asilimia 90.7, ikiwa 89.2 ya mjini na vijijini.
Maeneo ya mijini waliandikishwa asilimia 95.3 ikiwa 95.1 ni wa kiume na 95.5 wa
kike. Maeneo ya vijijini waliandikishwa asilimia 89.4 ikiwa 87.6 wa kiume na
91.3 wa kike”.
Kwa upande wa mkoa wa Njombe,
waliandikishwa wanafunzi asilimia 89.7, ikiwa 88.0 ni wa kiume na 91.3 wa kike.
Kwa maeneo ya mijini waliandikishwa asilimia 93.9 ikiwa 93.7 ni wa kiume na
94.1 wa kike. Maeneo ya vijijini waliandikishwa asilimia 88.6 ikiwa 86.6 wa
kiume na 90.6 wa kike.
Katika ajira, Bw. Fundi amesema “mkoa
wa Iringa unaweza kutoa ajira katika sekta rasmi za umma na binafsi kwa kuajiri
jumla ya watu 4,936 ikiwa wanaume 2,501 na wanawake 2,435”. Amesema mkoa wa
Njombe, umeweza kutoa ajira katika sekta rasmi za umma na binafsi na kuajiri
jumla ya watu 1,319 ikiwa wanaume 698 na wanawake 621.
Mikoa ya Iringa na Njombe kwa pamoja
ina pato la Tshs. Milioni 2,347.081 kwa mwaka 2012 na Tshs. Milioni 2,755,924
kwa mwaka 2013. Wakati pato la mkazi ni Tshs. 1,428,243 kwa mwaka 2012 na Tshs.
1,660,532 kwa mwaka 2013.
Mkoa wa Iringa una wakazi 941,238 wakati
Njombe ukiwa na wakazi 702,097.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni