MWENGE wa Uhuru utawasili
Mkoani Iringa tarehe 22 Juni, 2015 na kukimbizwa hadi tarehe 26 Juni, 2015.
Katika taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza jana
kuhusu ratiba na shughuli za mbio za mwenge wa uhuru mkoani Iringa.
Mkuu
wa Mkoa amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utapokelewa kutoka Mkoa wa Morogoro tarehe
22 Juni, 2015. Makabidhiano yatafanyika katika kijiji cha Ruahambuyuni kuanzia
saa 2.00 hadi saa 3.00. asubuhi.
Akiongelea
ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Mkoa amesema
kuwa katika Mkoa wa Iringa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaanza Wilaya ya Kilolo
tarehe 22 Juni 2015, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 23 Juni, 2015,
Manispaa ya Iringa tarehe 24 Juni 2015 na Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi
tarehe 25 June, 2015 ambapo Mwenge wa Uhuru utakuwa umekamilisha Mbio zake
katika Mkoa wa Iringa.
Mkoa
wa Iringa utaukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Njombe tarehe 26 June, 2015
katika eneo la Makambako kijiji cha Idofi.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa amezitaja shughuli ambazo zitafanywa na Mwenge wa Uhuru
katika Mkoa wa Iringa kuwa ni kuweka mawe ya msingi, utakagua, utazindua na
kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 35 yote ikiwa na thamani ya shillingi.4,985,562,793/= ambapo kati ya
fedha hizo Serikali kuu imechangia shilingi 2,193,787,197/= Halmashauri za Wilaya na Manispaa shilingi.1,191,486,781/= michango ya
wananchi shilingi 1,158,299,859/= na wadau wa maendeleo shilingi 441,988,956/=.
Mheshimiwa
Masenza ameutaja ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2015
”Tumia
Haki yako ya Kidemokrasia; chini ya kauli mbiu; jiandikishe na kupiga kura
katika uchaguzi wa mwaka 2015’’
Mwenge wa Uhuru kila mwaka hubeba ujumbe wa
kudumu ambao ni:- ‘Mapambano dhidi ya
Rushwa ; kata mnyororo wa rushwa chini ya kauli mbiu’’ chagua kiongozi
mzalendo’’,
‘Mapambao dhidi ya dawa za kulevya; uteja
wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chini ya kauli mbiu ’’chukua hatua’’
Mapambao dhidi ya UKIMWI; Vijana wa leo na
UKIMWI chini ya kauli Mbiu ’’wazazi tuwajibike’’
Mapambano dhidi ya Maralia; Wekeza katika
maisha ya baadae; chini ya kauli mbiu ’’tokomeza malaria’’
Ametoa
wito kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari kuwahamasishwa wananchi
katika Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge
wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki katika mikesha ya Mwenge
pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2015.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni