Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkuu
wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza amepongeza kazi za kijamii zinazofanywa na
muwekezaji Geoff Fox kwa lengo la kuwapunguzia umasikini wananchi wa Mufindi.
Pongezi
hizo alizitoa alipotembelea shughuli za maendeleo zinazofanywa na muwekezaji
huyo wilayani Mufindi kwa lengo la kujifunza pamoja na kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa. “Nimefurahishwa na kazi za kijamii zinazofanywa na muwekezaji
za kuisaidia jamii katika sekta za afya, elimu na ustawi wa jamii. Kazi hizi ni
jukumu letu kama serikali lakini kutokana na sera yetu ya ushirikishaji jamii
na sekta binafsi, sekta binafsi inapata fursa ya kusaidia juhudi hizi za
kimaendeleo” alisema Masenza.
Alipotembelea
zahanati ya Mdabulo inayomilikiwa na kanisa katoliki Jimbo la Iringa, mkuu wa
mkoa alipongeza kazi nzuri inayoendelea kufanywa na zahanati hiyo iliyoanzishwa
mwaka 1946 ikiwa umbali wa km 48 kutoka mjini Mafinga. Masenza alishauri
uandaliwe utaratibu wa kutoa elimu ya magonjwa ya kisukari na saratani na
mlango wa kizazi kutokana na magonjwa hayo kutokupewa kipaumbele. “Magonjwa ya
kisukari na saratani ya mlango wa kikazi yamekuwa hayapewi umuhimu sana lakini
yanachangia sana katika vifo vya wananchi wetu. Ni vizuri mkaweka utaratibu wa
kuwa mnatoa elimu ya utambuzi na kujikinga na magonjwa haya ili kupunguza
hatari ya vifo” alisema Masenza. Masenza aliiagiza halmashauri kununua mitungi
…na siki ili kusaidia uchunguzi wa saratani hiyo.
Mkuu
wa mkoa aliwaagiza wataalamu wa sekta ya afya wa halmashauri ya wilaya ya
mufindi kuweka utaratibu wa kuitembelea zahanati ya Mdabulo mara kwa mara na
kutoa ushauri wa kitaalam.
Kutokana
na zahanati hiyo kuwahudumia wananchi wengi, mkuu wa mkoa alimuagiza mganga
mkuu wa mkoa kufuatilia mchakato wa kuipandisha hadhi zahanati ya Mdabulo kuwa kituo
cha afya ufanyike haraka…ili…
…
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni