Ijumaa, 10 Juni 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HALI YA UWEPO WA WATUMISHI HEWA, UTEKELEZAJI WA UPATIKANAJI WA MADAWATI NA UPATIKANAJI WA SUKARI MKOANI IRINGA TAREHE 10/06/2016




a)            HALI YA UWEPO WA WATUMISHI HEWA

Ndugu Waandishi wa Habari;
Mtakumbuka kuwa tarehe 18/04/2016 nilitoa taarifa kwa vyombo vya Habari juu ya hali ya uwepo wa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa. Katika taarifa hiyo nilieleza kuwa ili kujiridhisha na kuondolewa kabisa kwa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa nitaunda Timu ya Wataalam kwa ajili ya kupita katika Hospitali Teule zote za Wilaya na kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kuendelea kubaini iwapo wapo watumishi hewa ambao hawakubainishwa katika zoezi la awali. Aidha, niliahidi kutoa taarifa kwenu mara zoezi hilo litakapokamilika.

Timu niliyounda imekamilisha kazi yake tarehe 07/06/2016 na kunikabidhi taarifa yake. Kwa ufupi taarifa hiyo imebainisha masuala mbalimbali. Masuala hayo ni pamoja na:-

·          Uwepo wa watumishi hewa 169 katika Halmashauri ambao wamekuwa wakipokea mishahara pasipo kustahili kutokana na utoro, kustaafu na kufariki. Mchanganuo wa watumishi hao kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:-

NA
HALMASHAURI
WATORO
WASTAAFU
WALIOFARIKI
JUMLA
1.
IRINGA MC
16
3
1
20
2.
MUFINDI DC
32
45
13
90
3.
IRINGA DC
27
14
1
42
4.
KILOLO DC
8
-
-
8
5.
MAFINGA TC
8
5
-
9

JUMLA
87
67
15
169

Aidha, upotevu wa fedha kutokana na ulipaji wa mishahara isivyostahili umeisababishia Serikali hasara ya shilingi Milioni 364,028,910.80 kwa mchanganuo ufuatao:-

 
NA
HALMASHAURI
WATORO/KUFUKUZWA
WASTAAFU
WALIOFARIKI
JUMLA
1.
IRINGA MC
  33,414,538.22
  4,043,806.76
  1,074,293.00
  38,532,637.98
2.
MUFINDI DC
  75,791,712.68
51,189,945.71
33,444,401.25
 160,426,059.64
3.
IRINGA DC
  66,645,516.78
25,371,476.97
19,306,668.50
 111,323,662.25
4.
KILOLO DC
  47,224,015.40
-
-
   47,224,015.40
5.
MAFINGA TC
   3,589,727.42
  2,932,808.11
-
     6,522,535.53

JUMLA
226,665,510.50
83,538,037.55
53,825,362.75
 364,028,910.80

Ndugu Waandishi wa Habari;
Timu hiyo pia imebaini kuwa, katika Hospitali Teule ya Ilula inayotoa huduma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo lipo tatizo la fedha za mishahara isiyolipwa inayofikia kiasi cha Shilingi Milioni 151,583,969.00 kutorejeshwa Hazina tangu Januari 2008 hadi Februari, 2016. Fedha hiyo imetumika kwa shughuli za  uendeshaji wa Hosipitali Teule ya Wilaya ya Ilula  pasipo idhini ya Serikali. Fedha hiyo ilitumika kugharamia huduma za umeme, ununuzi wa dawa na kulipa mishahara ya watumishi ambao orodha yake haikuwa inafahamika na Serikali kinyume na taratibu. Mkoa unaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa katika taarifa ya Tume na ninaahidi kuendelea kutoa taarifa ya utekelezaji baada ya kuyafanyia kazi.

b)            UTEKELEZAJI WA UPATIKANAJI WA MADAWATI

Ndugu Waandishi wa Habari;
Mkoa una jumla ya shule za Msingi 478 na shule za Sekondari 107 zinazo milikiwa na Serikali.
Awali Mkoa ulikuwa na upungufu wa Madawati 29,347, ikiwa Madawati 26,046 ni upungufu katika shule za Msingi, na Madawati 3,301 ni upungufu katika shule za Sekondari.
Hadi kufikia tarehe 06/06/2016, Halmashauri zimetengeneza jumla ya Madawati 17,225 kwa ajiri ya shule za Msingi na Sekondari. Hivyo kubaki na upungufu wa Madawati 4,681.
Hadi kufikia tarehe 6/6/2016 Mkoa umetengeneza jumla ya Madawati 442 na bado jitihada zinafanyika kwa ajili ya kuongeza zaidi idadi hiyo.  

 
UTEKELEZAJI WA MADAWATI HADI TAREHE 06/06/2016
S/N
HALMASHAURI
IDADI YA WANAFUNZI
MAHITAJI
YALIYOPO
YANYOTENGENEZWA
UPUNGUFU HADI SASA


MSINGI
SEKONDARI
MSINGI
SEKONDARI
MSINGI
SEKONDARI
MSINGI
SEKONDARI
MSINGI
SEKONDARI
1.
IRINGA (M)
25,133
9,135
12,567
9,135
6,961
9,768
4,690
308
-
-
2.
IRINGA DC
57,531
15,269
27,992
15,269
21,965
14,509
10,189
760
-
-
3.
KILOLO
53,038
10,209
22,361
10,209
14,734
8786
2129
650
1925
-
4.
MUFINDI
52,723
11,954
17,594
11,954
23,018
15,599
-
200
425
242
5.
MAFINGA TC
15,383
671
7,719
4339
5,768
4398
217
60
1734
355


JUMLA

203,808

47,238

88,233

50,906

72,446

53,060

17,225

1978

4084

597

(C) HALI YA UPATIKANAJI WA SUKARI KATIKA MKOA WA IRINGA
Ndugu Waandishi wa Habari;
Mkoa wa Iringa hauna kiwanda cha uzalishaji wa sukari. Kutokana na kukosekana kwa uzalishaji wa sukari kwa Mkoa wetu tunategemea sukari inayozalishwa kutoka mikoa mingine. Sukari hiyo huletwa Mkoani hapa na Mawakala walioteuliwa na Bodi ya sukari. Mahitaji ya sukari kwa Mkoa wa Iringa kwa mwaka ni tani 14,000, kati ya tani hizo, Walaji wa kawaida hutumia tani 9,000 na matumizi ya viwanda ni tani 5,000.

i.                      Hali ya upatikanaji wa sukari
Changamoto ya upungufu wa sukari hapa Mkoani imeanza mwezi Machi, 2016 hadi sasa. Kabla ya huu mwezi changamoto haikuwepo na sukari ilikuwa inauzwa kwa bei ya jumla Tsh.88,000  kwa kg. 50 na bei ya reja reja ilikuwa inauzwa Tsh.1,800-2,000 kwa Manispaa ya Iringa na Tsh.2,000-2,200 Kwa Halmashauri za Wilaya hususan maeneo ya Vijijini. Kwa sasa inauzwa kwa bei ya jumla Tsh.110,000  kwa kg. 50 na bei ya rejareja inauzwa kati ya Tsh.2, 800 na Tshs. 3,000 kwa Manispaa ya Iringa, na Tsh.3,000-3,400 kwa Halmashauri za Wilaya na maeneo ya Vijijini. 

ii.                    Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na upungufu wa Sukari
Ø  Kuhamasisha Mawakala wa sukari kuleta sukari nyingi.
Ø  Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini wanaouza bei ya juu na kuchukua hatua stahiki.

Ndugu Waandishi wa Habari;
Nichukue nafasi hii kuwatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Iringa na hasa waumini wa dini ya Kiislamu ambao wameanza mfungo mtukufu wa Ramadhani kuwa, katika kipindi chote cha Mfungo Mtukufu na baada ya mfungo kuwa sukari itaendelea kupatikana. Mawakala wataendelea kuleta Sukari ya kutosha kukidhi mahitaji ya wananchi. 

Asanteni kwa kunisikiliza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...