Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Halmashauri
ya Wilaya ya Iringa inajivunia nguvukazi ya vijana katika kujiletea maendeleo
na maendeleo ya Halmashauri hiyo kwa ujumla.
Akifafanua
nafasi ya nguvukazi ya vijana katika Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka wakati wa mbio za Mwenge wa
uhuru katika Halmashauri yake, alisema kuwa jumla ya vijana 1,321 wametumika na
kupata ajira katika miradi ya kijamii.
Aliongeza kuwa vijana wengine 1,230
walipata ajira kupitia makampuni yaliyopata zabuni za Halmashauri. Katika
miradi ya barabara ni vijana 1,200 (me 900 na ke 300), na miradi ya ujenzi wa
miundombinu ya umwagiliaji vijana ni vijana 30 (me 24 na ke 6). Alisema kuwa
vijana 28,783 (me 11,781 na ke 16,877) wamewezeshwa kujiajiri na kuajiriwa.
Katika sekta ya kilimo vijana 26,730, shughuli za ujasiliamali 1,372 na
bodaboda 250.
Kisaka
alisema kuwa ekari 198 zimetengwa katika vijiji 10 vya Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa kwa ajili ya vijana kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Katika
kuimarisha na kuhakikisha upatikanaji wa mitaji, SACCOS tatu za vijana za
Iringa Vijana Saccos, Mangalali na Nduli zimeundwa kwa lengo la kusaidia na
kuwawezesha vijana kupata mikopo yenye masharti nafuu.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni