Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Jamii
imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya rushwa kwa kutoa
taarifa na ushirikiano kwa Takukuru ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati la uelimishaji mkoa wa Iringa, Anneth
Mwakatobe alipokuwa akielezea nafasi ya jamii katika kupambana na rushwa kwenye
maonesho ya shughuli za kuzuia na kupambana na rushwa katika uwanja wa mkesha
wa mwenge wa uhuru katika mji mdogo wa Ifunda wilyani Iringa.
Mwakatobe
alisema kuwa rushwa ni matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa mtumishi wa umma au
binafsi kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe hivyo ni jukumu la jamii nzima
kupambana na vitendo hivyo.
Akiongelea
madhara ya jamii kuogopa au kukataa kushirikiana na Takukuru kufichua au kutoa
ushahidi dhidi ya vitendo vya rushwa, alisema kuwa ni kuongezeka kwa vitendo
vya rushwa katika jamii ambapo waathirika wakubwa wa vitendo hivyo ni jamii
yenyewe. Madhara mengine ni mapambano ya rushwa kuwa magumu kwa Takukuru
kuachiwa yenyewe kupambana na rushwa na kuwapa nafasi watuhumiwa wa vitendo vya
rushwa kuendelea kujinufaisha.
Mwakatobe
alisema kuwa Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaaka 2007
iliongeza wigo wa kutosha kwa kuongeza makosa ya rushwa na kuipa takukuru meno
zaidi. Alisema kuwa kifungu cha 15 kosa la kupokea rushwa, kushawishi kupewa
rushwa, kutoa rushwa au kuahidi kutoa rushwa adhabu ni faini isiyopungua
shilingi 500,000 na isiyozidi 1,000,000. Aliongeza kuwa kufungo kisichopungua
miaka mitatu na kisichozidi miaka mitano au faini na kifungo kwa pamoja.
Alisema
kuwa Takukuru imejidhatiti kuijengea jamii tabia ya kukataa vitendo vya rushwa
kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo kwa kuanzisha klabu za wapinga
rushwa katika maeneo hayo.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni