Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Halmashauri
ya wilaya ya Iringa imekopesha zaidi ya shilingi milioni 80 kwa vikundi 34 vya
vijana kwa lengo la kukuza mtaji na kujiletea maeneleo kupitia shughuli za
ujasiliamali.
Akisoma
risala ya utii ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika mbio za Mwenge
wa uhuru, Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Olgato Mwinuka alisema
kuwa katika kipindi cha mwaka 2015/2016 Halmashauri hiyo ilikusanya mapato ya
ndani shilingi 1,201,059,165 na kutenga asilimia tano sawa na shilingi
85,724,000 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya vijana.
Alisema “jumla ya fedha zilizotolewa ni shilingi
87,000,000 kati ya fedha hizi kiasi cha shilingi 30,000,000 zilitokana na
asilimia tano ya mapato ya ndani, shilingi 37,000,000 zilitokana na mfuko wa
vijana wa Halmashauri na shilingi 20,000,000 zilitokana na mkopo kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo”.
Alisema kuwa fedha hizo
zilikopeshwa kwa vikundi 34 vya vijana vyenye jumla ya wanachama 361 (me 220 na
ke 130) na kufanya kazi za uendeshaji miradi ya vijana katika kilimo cha
mahindi, mpunga, alizeti, ufuta na mtama. Maeneo mengine aliyataja kuwa ni
uselemala, ushonaji na ufugaji wa samaki, kuku, mbuzi na kondoo.
Mwinuka
alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa imeanzisha jumla ya vikundi 197
vya uzalishaji mali vya vijana waliosajiliwa vyenye jumla ya wanachama 1,811
(me 1,077 na ke 734).
Alisema
kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali
ambayo yamewezesha vijana 651 (me 462 na ke 189) kupata mafunzo katika fani
mbalimbali za ujasiliamali, stadi za maisha, kujitambua na kujikinga na maambukizi
ya Ukimwi.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni