Na.
Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Halmashauri
za mikoa ya nyanda za juu kusini zimetakiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali
kutekeleza majukumu yao.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipotembelea
mabanda ya maonesho ya Halmashuri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
katika uwanja wa Nanenane mjini Mbeya.
Ayubu
alisema kuwa wasindikaji katika Halmashauri wasiachwe kufanya kazi za kusindika
bidhaa majumbani.
“Wasindikaji
wameshuhudia kuwa wanafanya kazi za usindikaji nyumbani badala ya kufanya kazi
hizo katika maeneo rasmi. Serikali likwisha zielekeza mamlaka za serikali za
mitaa kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali kuweza kutekeleza majukumu yao. Maeneo hayo lazima yawe yenye miundombinu ya maji na umeme na kufikika kwa
urahisi” alisisitiza Ayubu.
Aidha, aliongeza kuwa Halmashauri ziwasaidie wajasiriamali
kufikia viwango vya ubora unaotakiwa na kuwasaidia kupata nembo ya ubora ya TBS
na ‘Bar cord’ ili kuweza kupata soko la ndani na nje ya nchi.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni