Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Iringa
Serikali
imesisitiza kuwa uchumi wa viwanda nchini unategemea sana viwanda vidogo vidogo
vilivyopo katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipotembelea
mabanda ya maonesho ya Nanenane mjini Mbeya jana.
Ayubu
alisema kuwa uchumi wa viwanda unategea sana viwanda vidogo vidogo ambavyo
msingi wake ni wajasiriamali wadogo. Alisema kuwa uzalishaji wa bidhaa za wajasiriamali
wadogo una mchango mkubwa kwa nchi inapoelekea katika uchumi wa kati.
“Wajasiriamali
msikate tamaa, fanyeni kazi kwa juhudi zaidi, serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais Dk John Magufuli ipo nyuma yenu kuhakikisha inawatengenezea mazingira
mazuri ya kufanyia kazi” alisisitiza Ayubu.
Aliongeza kuwa watanzania wapo
tayari kununua bidhaa za ndani kwa lengo la kukuza uchumi wa wajasiriamali na
taifa kwa ujumla. Changamoto iliyobaki ni kuhakikisha bidhaa zinakuwa na ubora
unaokubalika kwa kuhakikisha zinakuwa na nembo ya ubora ya TBS na ‘Bar
cord’.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni