Na. Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Iringa
Vyama
vya ushirika katika mikoa ya nyanda za juu kusini vimetakiwa kushikamana katika
kukuza ushirikiano na mtaji.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipotembelea banda la Manispaa
ya Iringa katika maonesho ya Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale mjini Mbeya.
Mheshimiwa Masenza
alisema kuwa wanaushirika wanatakiwa kushikamana ili kuimarisha umoja na kukuza
mtaji wao. “Wanaushirika mnapopotezana,
ushirika unaparaganyika. Wanaushirika tushikaname ili kudumisha ushirika hasa
kina mama” alisema mheshimiwa Masenza.
Mheshimiwa Masenza
alisema kuwa vijana wamekuwa wagumu kujiunga na vyama vya ushirika na kuwaacha
watu wazima na wazee katika sekta ya ushirika. Aliwataka wanaushirika kubuni
mbinu za kuwavutia vijana ili wajiunge na ushirika.
Wakati
huohuo, mkuu wa mkoa aliwasisitiza wakina mama kuonesha ushupavu katika
ushirika kusimamia na kuimarisha ushirika. Aliwashauri wakina mama kuanzisha
tawi B katika ushirika kwa ajili ya watoto wao ili kuwarithisha dhana ya
ushirika.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni