Na Mwandishi Maalum, Iringa
Vyombo
vya habari katika mikoa ya nyanda za juu kusini vimetakiwa kutangaza maandalizi
ya maonesho ya Utalii Karibu Kusini na maonesho ya shughuli za viwanda ili
kuwaletea maendeleo wananchi wa kanda hiyo.
Wito
huo ulitolewa na mwenyekiti wa kikao cha viongozi wakuu wa mikoa ya nyanda za
juu kusini katika maandalizi ya maadhimisho ya maonesho ya Utalii Karibu Kusini
na maonesho ya shughuli za viwanda vidogo (SIDO), mheshimiwa Amina Masenza katika kikao
kilichofanyika hifadhi ya taifa ya Ruaha jana.
Mheshimiwa Masenza
ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa vyombo vya habari katika
mikoa ya nyanda za juu kusini vina mchango mkubwa katika kufanikisha maonesho
ya Utalii Karibu Kusini na maonesho ya shughuli za viwanda vidogo (SIDO).
“Waandishi wa habari mna jukumu muhimu katika
kufanikisha shughuli hii. Nawaomba mtusaidie kutangaza Utalii Karibu Kusini na
shughuli za viwanda vidogo” alisema mheshimiwa Masenza.
Wakuu
wa mikoa ya nyanda za juu kusini walioshiri ziara hiyo ni mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Galawa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na mkuu wa mkoa wa Njombe.
Maonesho
ya Utalii yatafanyika pamoja na Maonesho shughuli za Viwanda Vidogo (SIDO)
kanda ya nyanda za juu kusini kwa Mwaka 2017.
Maonesho haya yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 29/09/2017 hadi tarehe
02/10/2017.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni