Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa- IRINGA
Kampeni
tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza inalenga kutoa elimu kwa
jamii na kupima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ili matibabu yaweze kuanza
mapema.
Kauli
hiyo ilitolewa na daktari bingwa wa kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu
kutoka hospitali ya Kibong’oto Dr. Isaya Jelly alipokuwa akiongea na wanahabari
mkoani Iringa kuhusu kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza
katika bustani ya Manispaa ya Iringa.
Dr.
Jelly ambae pia anaratibu shughuli za shiriki la Save the Children kupitia
mpango wa Taifa wa kifua kikuu na ukoma (NTLP) alisema kuwa kampeni hiyo
imelenga kuwasogeza wananchi karibu na huduma za upimaji na tiba.
“Kampeni hii imelenga kuwasogeza karibu
wananchi kupata habari na kupima kama wanavimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na
kuanza dawa” alisema Dr. Jelly.
Dr.
Jelly alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kampeni hiyo ni mzuri. “Hali ya kimaisha inafanya watu wasizifuate
huduma katika vituo vya afya, kwa kuongopa mlolongo uliopo katika vituo vya
huduma. Huduma za hapa uwanjani ni za haraka haraka” alisema Dr. Jelly.
Alisema kuwa wananchi watakao pima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu baada ya
uchunguzi majibu yao watatumiwa kupitia simu zao za mkononi. Aidha, kwa
wananchi watakaopima virusi vya ukimwi majibu watapewa baada ya kupewa somo la
kuwekwa sawa kisaikilojia.
Katika
kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza, imelenga kuwafikia
wagonjwa 100 katika Manispaa ya Iringa na zoezi hilo litaelekea katika gereza la
Iringa kesho kwa ajili ya kuwapima na kuwaanzishia tiba wanaorekebishwa tabia
watakaogundulika na vimelea vya kifua kikuu.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni