Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa-IRINGA
Vyama
vya siasa mkoani Iringa vimetakiwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuachana na
vitendo vya vurugu kwa sababu serikalai ipo macho muda wote.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa
akiongea katika kipindi cha Sunrise power kinachorushwa na kituo cha redio Nuru
cha mjini Iringa jana.
Mheshimiwa
Masenza ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa
alivitaka vyama vya siasa kuendesha kampeni za kistaarabu katika maeneo
utakapofanyika uchaguzi mdogo wa madiwani.
“Napenda
mkubuke kuwa baada ya uchaguzi maisha yanaendelea kama kawaida. Kila chama
lazima kipige kampeni kwa uhuru na ustaarabu bila kusababisha viashiria vya
vurugu” alisema mheshimiwa Masenza.
Aliongeza kuwa mtu yeyote atakayefanya
vurugu afahamu kuwa serikali ipo macho itamshughulikia kwa mujibu wa sheria za
nchi.
Uchaguzi
mdogo wa madiwani unatarajiwa kufanyika tarehe 26/11/2017 katika Kata za
Kitwiru na Kimala katika halmashauri za Manispaa na Kilolo mtawalia katika mkoa
wa Iringa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni