Na.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mamlaka za serikali
za mitaa na wadau wa maendeleo wametakiwa kuwatumia maafisa habari wa serikali
katika kuhabarisha utekelezaji wa miradi ili wananchi waweze kunufaika na
huduma zao.
Kauli hiyo
ilitolewa na mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr Atupele Mwandiga
alipokuwa akifunga kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa
wadau wa Mkoa wa Iringa katika hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa jana.
Dr Mwandiga alisema
kuwa mafanikio ya miradi inayotekelezwa kwa wananchi yanategemea na utoaji na
upatikanaji wa taarifa za huduma zinazotolewa.
“Vivyo, hivyo mafanikio ya mradi huu wa ‘USAID Tulonge Afya’ pamoja na
mambo mengine utategemea sana upatikanaji na ubadilishanaji wa taarifa za
huduma na mafanikio. Na hili ni jukumu la maafisa habari wa serikali. Bahati
nzuri kwa Mkoa wetu wa Iringa, serikali imeajiri maafisa habari katika ngazi ya
Mkoa na Halmashauri zote. Ni matumaini yangu kuwa wataalamu hawa watatumika
vizuri katika kufikia malengo ya mradi huu” alisema Dr Mwandiga.
Aidha,
aliwataka kuwatumia pia maafisa maendeleo ya jamii walio katika kata zote za Mkoa
wa Iringa katika kutekeleza mradi huo.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni