Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa mkoani Iringa watakiwa
kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Rais ya utoaji wa elimu bila malipo mkoani
hapa.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiongea na
walimu wakuu na wakuu wa shule katika kikao maalum cha kujiridhisha na
utekelezaji wa maagizo ya Rais juu ya elimu bila malipo kilichofanyika katika
shule ya sekondari Lugalo leo.
“Niwaagize wakuu wa Wilaya kama yapo mambo
kama hayo yanaendelea katika Wilaya zenu na nyie hamjui na hamjaniambia nayie
mtakuwa mnanihujimu. Sasa nisingependa tabia ya kuhujumiana ikawa sehemu ya
utawala katika Mkoa wetu” alisema Masenza.
Aidha,
aliwataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikalai za Mitaa kusimamia shule katika
Halmashauri zao ili suala la uchangishaji michango kinyume na maelekezo
usiwepo.
Alisema
kuwa kikao hicho ni kikao cha kujiridhisha kama kuna shule inayoendesha
michango na inasimamiwa na mwalimu. Alisema kuwa mwisho wa kikao hicho kila
mkuu wa shule awe ameandika barua kumueleza mkuu wa Mkoa juu ya hali ya jambo
hilo.
Aidha,
mkuu wa Mkoa aliagiza kuwa kwenye elimu bure hakuna michango, na kupiga
marufuku kwa mwalimu yeyote kuchangisha mchango na kuwarudisha nyumbani
wanafunzi kwa kisingizio cha michango. Aidha, alipiga marufuku wanafunzi wote
wanaoripoti shuleni kurudishwa nyumbani kwa kutokuwa na sare.
Wakati
huohuo, amezitaka shule binafsi kuacha mara moja kukaririsha vidato wanafunzi
wasiofikia wastani na kwamba shule zitakazokiuka agizo hilo zitafutiwa usajili.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni