Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
MKUU
wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wakuu wa shule za sekondari na msingi
kuthibitisha kwa barua iwapo kuna michango yeyote inayoendelea katika shule zao
kinyume na maelekezo ya serikali.
Agizo
hilo amelitoa leo katika kikao cha dharura na wakuu wa shule na walimu wakuu
kufuatia agizo la Rais w Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa jana kuhusu
michango katika shule nchini.
“Serikali imekwisha elekeza kuwa tunakwenda
na elimu bila malipo. Mtu yeyote nayekwenda kinyume na hilo anakwenda kinyume
na maelekezo ya serikali. Ni Rais aliyetoa amri hii yeye ndiye mwenye usemi wa
mwisho katika mambo yote ya Taifa hili. Yeyote anayekiuka hili atakuwa anafanya
kwa dharau” alisema Masenza.
Alisema
kuwa waraka wa elimu Namba 3 wa mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa elimu ya
msingi bila malipo ulitoa maelekezo ya utekelezaji wa jambo hilo.
Alisema
kuwa alikwisha kuwa iwapo kuna hitaji lolote katika shule, libainishwe na jamii
na jamii yenyewe ndiyo isimamie utekelezaji wa jambo hilo nje ya utaratibu wa
mwalimu mkuu na walimu wengine.
“Nimewaita hapa nijiridhishe, nitamtaka kila
mwalimu mkuu wa shule ya msingi na sekondari kwa mkono wake aandike barua kwa
mkuu wa Mkoa kuthibitisha kwamba ama upo mchango unaoendelea katika shule yake
ama hakuna. Barua zenu zote tutazipitia moja baada ya nyingine. Baada ya hapo
tutakuwa na ukaguzi na kuongea na bodi na kamati za shule ili zitumbie kama wanayo
michango, michango hiyo iliidhinishwa na nani, ni kiasi gani na kwa madhumuni
gani?” alihoji mkuu wa Mkoa.
Aliongeza
kuwa eneo lolote litakalobainika kuwa mwalimu mkuu ndiye kichocheo cha huo
mchango na yeye ndiye anasimamia hafai na kwa tamko la Rais hana kazi.
Mkuu
wa Mkoa aliwataka walimu hao kuacha kuchezea maagizo ya serikali. Aidha,
alionesha kuwashangaa waratibu wa elimu ambao katika maeneo yao kuna michango
inayoendelea na wao hawafahamu. Aidha, aliwaelekeza waratibu hao kuwepo katika
vikao vya bodi na kamati za shule ili kufahamu hli ya mambo inavyokwenda.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni