Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Iringa
Kamati
ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa imehakikishiwa kufanya kazi kwa amani
na usalama mkoani Iringa kutokana na vyombo vya usalama kuwa macho muda wote.
Uhakika
huo ulitolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa,
Amina Masenza alipokuwa akiongea na kamati ya Bunge ya utawala na serikali za
mitaa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kamati hiyo ilipofanya ziara
mkoani hapa.
Masenza
ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa upo shwari.
Hali ya usalama ni nzuri kuiwezesha kamati hiyo kufanya ziara ya kikazi katika
hali ya usalama na utulivu. Aidha, aliongeza kuwa wananchi mkoani Iringa
wanajitambua katika kutekeleza majukumu yao.
“Wananchi mkoani Iringa hasa wakulima katika msimu huu wa kilimo
wanajitambua na hawashurutishwi kutekeleza majukumu yao ya kilimo” alisema
Masenza.
Wakati
huohuo, makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa,
Mwanne Mchemba alisema kuwa dhumuni la ziara ya kamati yake ni kukagua miradi
ya maendeleo wilayani Kilolo kwa fedha zilizotolewa na serikali mwaka
2016/2017.
“Tunajua kuwa mkuu wa Mkoa ni
jembe katika usimamizi wa uhamasishajai wa maendeleo. Hivyo, kamati inataka
kujiridhisha na matumizi ya fedha za serikalai hasa thamani ya fedha kabla ya
serikali kuidhinisha fedha nyingine kwa Wilaya ya Kilolo” alisema
Mchemba.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni