Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amefurahishwa na utaratibu wa kurithisha mbinu
za ufugaja kwa wanafunzi kwa lengo la kuwajengea moyo wa kuwajibika wanafunzi
wanufaika wa mpango wa TASAF wilayani Mufindi.
Masenza
alisema hayo alipokuwa akiongea na wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya
masikini na wanafunzi wanaonufaika na fedha za elimu kupitia TASAF katika shule
ya msingi Mafinga iliyopo mjini Mafinga jana.
Masenza
alisema kuwa utaratibu wa kuwafundisha watoto wadogo ufugaji wa mifugo wadogo
kama kuku ni jambo zuri. Alisema kuwa utaratibu huo unawaandaa watoto hao
kuweza kujitegea wanapokuwa na kuondoa utegemezi kwa jamii inayowazunguka.
Aidha, alitoa wito kwa wanufaika wengine wa mpango wa TASAF na jamii kwa ujumla
kuiga utaratibu huo.
Awali
mwanafunzi mnufaika wa shule ya msingi Mafinga, Hosana Chaula aliishukuru
serikali kwa kuanzisha mpango wa kunusuru kaya masikini. Alisema kupitia mpango
huo ameweza kununuliwa vifaa na sare za shule.
“Pia nilinunuliwa kuku 4 nikawahudumia na wakatotoa vifaranga 10. Kati
ya vifaranga hivyo, vifaranga vitano vilikufa” alisema Chaula.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni