Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wizara
ya maliasili na utalii imepongezwa kwa kuunga mkono juhudi za kuendeleza utalii
Mkoa wa Iringa.
Pongezi
hizo zilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipotoa salamu za Mkoa
katika kikao cha tatu cha kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu kilichofanyika
katika ukumbi wa chuo cha VETA mjini Iringa jana.
Masenza
alisema kuwa wizara imekuwa ikiunga mkono juhudi za kuendeleza utalii kwa Mkoa
wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini. “Pongezi kwa juhudi za wizara ya
maliasili na utalii kuunga mkono juhudi za kuendeleza utalii mkoani Iringa”
alisema Masenza.
Aidha, alimhakikishia waziri wa maliasili na utalii kuwa Mkoa
wa Iringa umejipata vizuri katika kukuza na kuendeleza utalii kwa ukanda wa
kusini.
Mkuu
wa Mkoa alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa utalii unakuwa endelevu, Mkoa wa Iringa
umefanya utalii kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyake. Alisema kuwa Mkoa
umejipanga kuendeleza eneo la Kihesa kilolo kwa kukuza utalii kwa kulitunza,
kuliendeleza na kulihifadhi. Utunzaji wa eneo hilo utachangia uendelevu wa sekta
ya utalii na uhifadhi mkoani Iringa na ukanda wa nyanda za juu kusini, alisema
mkuu wa Mkoa.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni