Serikali imelitaka baraza la usimamizi wa mazingira (NEMC)
kufanya upya tathmini ya athari za kimazingira katika eneo la Igumbilo
inapotarajiwa kujengwa stendi mpya ya mabasi na halmashauri ya Manispaa ya
Iringa.
Waziri wa Nchi OMR- Mazingira Dkt. Binilith Mahenge (wa tatu kushoto)
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais- Mazingira, Dkt. Binilith Mahenge alipofanya ziara ya kutembelea eneo
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya mabasi mjini Iringa.
Dkt. Mahenge amelitaka baraza la usimamizi wa mazingira
kufanya upya tathmini juu ya athari za kimazingira na kuwasilisha taarifa hiko
kwake. Kauli hiyo imekuja kutokana na mvutano wa muda mrefu sasa baina ya
Manispaa ya Iringa na wadau wa maji kwamba mradi huo itaharibu chanzo pekee ya
chaji katika mji wa Iringa. Aidha, Dkt. Mahenge amesema kuwa katika kipindi
chote Manispaa ya Iringa isifanye shughuli zozote za maendeleo katika eneo hilo.
Waziri wa Nchi OMR amesema kuwa lengo la kutembelea eneo la
Igumbilo ni kujionea hali halisi kufuatia hoja zilizotolewa na wadau mbalimbali
hasa wa maji kuhusu ujenzi wa stendi hiyo. Amesema kuwa baada ya tathmini hiyo
wataalam watamshauri kitaalam kwa mujibu wa taaluma. Amesema kuwa maamuzi ya
kitaaluma hayawezi kufanywa kisiasa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Gervas Ndaki litaka suala
hilo lisichukuliwe kisiasa. Amesmea kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara
wanaopinga kwa nguvu dhana ya stendi hiyo kuhamishwa mjini na kujengwa eneo la
Igumbilo kutokana na maslahi yao ya kibiashara.
Katika taarifa fupi ya mkoa wa iringa iliyowasilsihwa kwa
Waziri wa nchi OMR na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu amesema kuwa
mradi wa ujenzi wa stendi, unatokana uhitaji mkubwa wa uboreshaji wa
miundombinu ya usafiri katika manispaa ya Iringa na mkoa kwa ujumla.
Amesema
lengo la ujenzi wa stendi mpya ni kuboresha muindombinu ya stendi ndani ya mji
kutokana na misongamano mikubwa katikati ya mji na kukosa nafasi ya kupanua
stendi. Amesema kuwa halmashauri hiyo kwa kujenga stendi hiyo inakusudia
kuongeza kuboresha vyanzo vya mapato na kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii
kwa wananchi wake.
Akiongelea sheria
iliyoanzisha mamlaka za maji, Ayubu amesema kuwa sheria hiyo inazitaka mamlaka
kusambaza kwa wananchi maji yaliyo safi na salama. Amesema kuwa ikitokea
mamlaka imewasambazia wananchi maji ambayo hayako katika viwango mamlaka
itakuwa inakiuka sheria. Amesema kuwa wananchi wa manispaa ya Iringa watakuwa
kwenye mazingira hatarishi kwa kunywa maji yenye takakemikali na kupelekea
madhara kiafya.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma akiongea na waandishi wa Habari
Chanzo cha maji
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni