Jumapili, 16 Machi 2014

USALAMA WAHAKIKISHWA KATIKA UCHAGUZI WA JIMBO LA KALENGA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
MKUU wa Mkoa wa Iringa amewataka wananchi wa jimbo la Kalenga kujitokeza kwa wingi kupiga kura za kumchagua mbunge wa jimbo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiongea na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa Mbunge wa jimbo la Kalenga ofisi kwake.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma ameitoa alipoongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea hali halisi katika jimbo la uchaguzi la Kalenga na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kumchagua mbunge katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 16/03/2014.

Akiongelea ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Mkoa wa Iringa amewahakikishia wananchi kuwa ulinzi utakuwepo wa kutosha na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha amani na usalama kwa wananchi katika kipindi chote cha kupiga kura na wakati wa kutoa matokeo.

Dkt. Ishengoma amesema kuwa maandalizi yamekamilika na vifaa vyote vinavyohitajika vimefika katika vituo vya kupigia kura. Amesema kuwa vituo vyote vitakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi jioni kwa muda uliopangwa.
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...