OFISI YA MKUU WA MKOA
Sekta ya kilimo inachangia
asilimia kubwa katika maendeleo ya taifa na kuajiri watu wengi zaidi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine
Ishengoma katika kongamano kati ya serikali na wadau kuhusu siku ya kilimo na
usalama wa chakula afrika lililofanyika katika kijiji cha Kaning’ombe wilayani
Iringa.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma aliyemuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Dkt. Bilal amesema “kama
tujuavyo kilimo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa taifa letu. Kilimo hutegemewa na
watanzania wengi hasa akina mama, na asilimia 75 ya kipato cha watanzania
hutokana na kilimo”. Amesema kuwa kilimo kinasaidia kwa kiasi kikubwa katika
ukuaji wa uchumi wan chi (GDP). Akiongelea umasikini, amesema kuwa pamoja na
ukweli kwamba umasikini bado upo nchini kilimo ni suluhisho la mabadiliko kwa
watanzania wengi. Amesema kwa msingi huo ni vizuri dira na malengo yaelekezwe
katika kilimo cha kibiashara.
Makamu wa Rais amesema kuwa
elimu ya uzalishaji bora wenye tija kwa wakulima wadogo itolewe ili waondokane
na umasikini. Amesema kuwa kufanya hivyo uchumi wan chi utazidi kukua na
kuongezeka kwa ustawi wa jamii.
Dkt. Bilal amesema kuwa
serikali itaendelea na jitihada za kuendeleza na kuimarisha sekta ya kilimo
nchini. Amesema program ya kuendeleza sekta ya kilimo ilizinduliwa rasmi mwaka
2005/2006 ambapo malengo makubwa ya program hiyo ni kuhakikisha kilimo kinakua
kwa asilimia 6 kwa mwaka. Amesema hadi sasa lengo halijafikiwa sababu ukuaji
bado ni asilimia 4 tu.
Amesema malengo
ya hayawezi kufikiwa bila kuunganisha nguvu na jitihada za pamoja. Ameseme
kupitia mkakati wa kilimo kwanza, serikali inaendelea kusimamia na kutekeleza
malengo iliyojiwekea na kwa kuzishirikisha sekta binafsi ili kuleta mafanikio
makubwa kwa pamoja.
Akiongelea
makubaliano na ahadi za Maputo mwaka 2003, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la
wadau wa kilimo (ANSAF), Audax Rukonge amesema kuwa katika kilele cha mkutano
wa umoja wan chi za Afrika, AU mwaka 2003 wakuu wan chi walikubaliana kuwa kila
nchi itenge kiasi cha asilimia 10 ya bajeti ya kitaifa iingizwe kwenye kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa kilimo (ANSAF), Audax Rukonge |
Amesema
kuwa kiwango hicho kilitarajiwa kutosha kuchangia kuongeza uzalishaji na tija,
kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 6 kwa mwaka na kuondoa tatizo la njaa na
umasikini. Amesema kuwa miaka kumi baadae ni nchi nane tu za Afrika zimetimiza
ahadi hiyo na kilimo katika nchi hizo kimekua kwa asilimia 6 na zaidi.
Amesema
kuwa unahitajika mtazamo mpya wa kibiashara dhidi ya kilimo tofauti na kisiasa
kwa kuwekeza maeneo ya kimkakati na yenye ufanisi mkubwa.
Kongamano
hili ni fursa ya kuhakikisha yanapatikana mafanikio katika kilimo kwa
kuzikabili changamoto mbalimbali kwa kuzifanyia kazi ili kupata mazao bora
yenye tija.
Aidha, ni muendelezo wa Kongamano la Umoja wa Bara la Afrika
uliozinduliwa na Rais Yayi Boni wa Benini, Mwaka 2012, katika kuendeleza Kilimo
na Usalama wa chakula ili kupata chakula
cha uhakika.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni