Jumapili, 16 Machi 2014

MASTER PLAN YA IRINGA YAANDALIWA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SERIKALI imedhamiria kuona mji wa Iringa unakuwa na kuwa na maendeleo endelevu kwa ustawi wa kwa kuandaa mipango shirikishi kwa wananchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita (GG) akifungua mkutano

Kauli hiyoimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa maandalizi ya mpango kamambe wa mji wa Iringa (Iringa Master Plan) iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita.

Dkt. Ishengoma amesema “lengo kuu la kuandaa mpango kamambe ni kuwezesha ukuaji wa mji ambao ni endelevu katika Nyanja za kiafya, usalama, mpangilio mzuri, muonekano mzuri na ustawi wa jamii”. Amesema kuwa katika kufanikisha mpango huo, ushirikishaji mipango iliyopita na inayoendelea ya kisera katika ngazi mbalimbali za utendaji utazingatiwa.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mpango kamambe husimamia uendeshaji wa mji kwa muda wa miaka 20. Amesema kuwa mpango huo unaweza kufanyiwa mapitio baada ya miaka mitano (5). Akiongelea umuhimu wa mpango amesema kuwa mpango hutoa mwongozo wa matumizi mbalimbali kwa ujumla kulingana na mahitaji ya jamii husika. Ameyataja matumizi hayo kuwa ni makazi, biashara, viwanda, kilimo, ufugaji na matumizi mengineyo.

Akiongelea Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007 na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria nyinginezo, hifadhi ya mazingira husimamiwa na mamlaka ya upangaji kwa kushirikiana na wadau wa mji husika.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo (kulia) na Afisa Mipango Miji wa Manispaa, Immaculate Senje wakifuatilia mkutano wa wadau kujadili Master Plan ya Mji wa Iringa
=30=

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...