Jumapili, 16 Machi 2014

TANGAZO LA WIKI YA MAJI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


 OFISI YA MKUU WA MKOA WA IRINGA



TANGAZO LA WIKI YA MAJI
Wananchi wa Mkoa wa Iringa mnatangaziwa kuwa MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI yatafanyika kuanzia tarehe 16-22/03/2014.

Uzinduzi wa maadhimisho hayo utafanyika tarehe 17/3/2014 katika kijiji cha IHIMBO Wilayani KILOLO na Kilele kufanyika katika kijiji cha  IKUKA tarehe 22/03/2014.

Mgeni rasmi katika siku ya Uzinduzi atakuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa na katika Kilele atakuwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Kauli mbiu ya Maadhimisho haya ni UHAKIKA WA UPATIKANAJI WA MAJI NA NISHATI.

Maadhimisho hayo yataendelea kuadhimishwa katika wilaya zote za Mkoa wa Iringa. 

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika Maadhimisho ya wiki ya Maji. 


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA:

OFISI YA MKUU WA MKOA WA IRINGA
SLP 858
IRINGA
Tel: +255262702021/ +255262702191
Fax no: +255262702082
Email: ras@iringa.go.tz Website: iringa.go.tz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Habari zinazoendelea hivi sasa

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze k...