Na.
Dajari Mgidange, IRINGA
Wananchi wametakiwa
kujitokeza kwa winngi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo mbalimbali
utakayokimbizwa mkoani Iringa.
Wito huo umetolewa na Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Iringa mwaka
2014 ofisini kwake leo.
Dkt. Ishengoma amesema
kuwa ni vizuri wananchi wakajitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru pindi
utakapopita katika maeneo yao. Amesema “ninawasihi wananchi kuendela kudumisha
amani na utulivu wakati wote ambapo Mwenge wa Uhuru utakuwa ukikimbizwa katika
mkoa wetu na hata baada ya kuhitimisha mbio hizo katika mkoa wetu”.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma |
Akiongelea uhamasishaji
katika halmashauri, Mkuu wa Mkoa amesema “ninapenda kutumia
fursa hii kuviomba vyombo vya habari na ninyi waandishi wa habari
kuwahamasishwa wananchi katika halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza
kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki
katika mikesha ya Mwenge pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka
huu 2014”.
Amesema
kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Iringa utakagua, kuweka mawe ya
msingi, kufungua na kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo 42 yenye thamani ya
Tsh. 3,109,958,020/=. Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utatoa ujumbe katika
maeneo yote ambako utakimbizwa. Ameitaja miradi itakayotembelewa na Mwenge wa
Uhuru kuwa ni miradi ya barabara, elimu, afya, kilimo na ufugaji. Miradi
mengine ameitaja kuwa ni miradi ya vijana na wanawake na hifadhi ya mazingira.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2014 unaongozwa na ujumbe usemao “katiba ni sheria kuu ya nchi’’
wenye kauli mbiu isemayo ’ jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.
=30=
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni