WANANCHI wa
maeneo yanayozunguka mlima Kitonga, uliopo katika wilaya ya Kilolo, mkoani
Iringa wametakiwa kuutunza msitu huo kutochoma moto hovyo wala kukata miti
yake, ili kuepuka athari za kimazingira zilizoanza kujitokeza duniani.
Wito huo
umetolewa na afisa mipango wa wilaya ya Kilolo, Angelina Maridadi wakati
akisoma taarifa ya mradi wa kuhifadhi msiti wa Kitonga baada ya Mwenge wa
uhuru, kuzindua mradi huo.
Maridadi alisema
wilaya ya kilolo ni miongoni mwa wilaya zinazoathiriwa kwa kiasi kikubwa na
uharibifu wa mazingira jambo ambalo, lazima lipigiwe kelele ili jamii iachane
nalo.
“Wananchi wa
kilolo tusaidiane kuhifadhi mazi”
Alisema kuwa
kuanzishwa kwa mradi huo kumetokana na mkakati wa wilaya hiyo katika kuendelea
kuhifadhi misitu ya asili, kwa kusimamia sheria za kudhibiri uharibifu wa
mazingira na kuhamasha jamii kujali maeneo hayo.
Alisema, eneo
la msitu wa hifadhi Kitonga linamiti mingi ya asili aina ya miyombo na kwamba,
mradi huo unavihusisha vijiji vya vitatu vinavyozunguka eneo hilo.
Maridadi
alisema mpaka sasa tayari zimeanza kutumika sh milioni 59 kwa ajili ya
kuendeleza msitu huo, na kwamba wananchi wa maeneo husika ndio wasimamizi wakuu
wa maeneo hayo.
Akizindua mradi
huo, Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Rahel Kassanda aliisisitiza jamii
kuendelea kulinda misitu hiyo kwa kutoharibu mazingira ikiwemo tabia za kuchoma
moto na kukata miti hovyo.
Alisema misitu
ikihifadhiwa itasaidia kulinda vyanzo vya maji ambavyo vitaongeza uzalishaji wa
chakula katika maeneo hayo na kusaidia kuinua uchumi wa nchi.
Kassanda
alisema mkoa wa Iringa kwa miaka mingi umekuwa ukisifika kwa hatua za utunzaji
wa mazingira na kwamba, ikiwa misitu itaendelea kutunza unaweza kuendelea kuwa
na sifa hiyo.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni